Nenda kwa yaliyomo

Mwanza (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwanza mjini)


Jiji la Mwanza
Picha ya angani ya Mji wa Mwanza
Picha ya angani ya Mji wa Mwanza
Picha ya angani ya Mji wa Mwanza
Jiji la Mwanza is located in Tanzania
Jiji la Mwanza
Jiji la Mwanza
Majiranukta: 2°31′S 32°54′E / 2.517°S 32.900°E / -2.517; 32.900
Nchi Tanzania
Mkoa Mwanza
Wilaya Nyamagana
Ilemela
Serikali[1]
 - Aina ya serikali Jiji
 - Mstahiki Meya Sima Constantine Sima
 - Mkurugenzi wa Jiji Selemani Yahaya Sekiete
Eneo
 - Jumla 256 km²
 - Kavu 184 km² 
 - Maji 72 km² 
Mwinuko 1,140 m (3,737.7 ft)
Idadi ya wakazi (2022)https://www.nbs.go.tz.
 - Wakazi kwa ujumla 1,004,521
EAT (UTC+3)
Kodi ya simu 028
Tovuti:  Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Wilaya za Jiji la Mwanza

Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 706,453 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).[2]: 173  Mwaka 2022 walihesabiwa 1,004,521 [3].

Jiji hili limekuwa na vivutio mbalimbali vikiwemo mawe yaliyo katika Ziwa Victoria katika eneo la Nyanza. Pia jirani kuna hifadhi za wanyama wa porini kama Sanane, ambapo kuna wanyama kama simba, swala, pundamilia, sokwe,duma na chui

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mwanza ilianzishwa na Wajerumani wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mahali paliteuliwa kutokana na nafasi ya bandari asilia upande wa kusini ya Ziwa Viktoria. Wajerumani waliuita mji kwa jina "Muansa" inaaminiwa ilikuwa matamshi yao ya neno "nyanza". Walijenga boma kubwa iliyoendelea kitovu cha mji. Takwimu ya Kijerumani ya 1912 ilihesabu wazungu 85, Wagoa 15, Wahindi wengine 300 na Waarabu 70 lakini haikutaja wakazi Waafrika. Palikuwa na makampuni ya biashara 12 ya kizungu na 50 ya Wahindi.[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Halmashauri ya Jiji la Mwanza". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 3 Oktoba 2022.
  2. "Ripoti ya Sensa 2012" (PDF) (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-03-26. Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  3. https://www.nbs.go.tz
  4. Koloniallexikon makala "Muansa"
Kata za Jiji la Mwanza - Mkoa wa Mwanza - Tanzania

Wilaya ya Ilemela: BugogwaBuhongwaBusweluButimba (Ilemela)IgomaIlemelaMkolaniNyakatoPasiansiSangabuye
Wilaya ya Nyamagana: IgogoIsamiloKirumbaKitangiriMbuganiMirongoMkuyuniNyamaganaNyamanoroPamba

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mwanza (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.