Nenda kwa yaliyomo

Vita vya Kagera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vita ya Uganda na Tanzania)
Mwalimu Julius Nyerere,1977
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Vita vya Kagera (kwa Kiingereza: kwa Kiingereza: Uganda-Tanzania War[1]) ni vita vilivyopigwa kati ya Uganda na Tanzania kuanzia tarehe 30 Oktoba 1978 hadi 11 Aprili 1979.

Vita hivyo vilihusu kugombania ardhi ya mkoa wa Kagera kati ya nchi ya Tanzania na Uganda.

Katika vita hivyo Tanzania, ikiongozwa na rais Julius Nyerere iliibuka kidedea kwa kuwapiga vema majeshi ya gaidi Idd Amini Dadah yaliyoungwa mkono wa Libya ya Muammar al-Gaddafi na pia Palestina ya Yasser Arafat.

Vita hivyo viliua watu karibu 5,000 na wengine kuachwa yatima.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzilishi wa vita hivyo alikuwa Iddi Amini Dadah aliyetaka kupewa na mwl. Nyerere ardhi ya Kagera, tena kwa shuruti ya kivita.

Nyerere aliwaongoza vema wanajeshi 100,000 wa Tanzania akisema, "mchokozi Iddi Amini Dadah ametuchokoza; uwezo wa kumpiga tunao, sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo, hivyo tumeamua kupambana naye". Aliungwa mkono na Msumbiji na wanaharakati wa Uganda, akiwemo Yoweri Museveni.

Katika vita hiyo Iddi Amini Dadah, baada ya kushambuliwa, alikimbilia nchini Libya, halafu Saudi Arabia hadi mauti yalipompata miaka ya baadaye.

Nchini Uganda ikawa ndiyo mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tanzania, iliyolaumiwa na Organization of African Unity kama kwamba ndiyo mvamizi, ililazimika kugharimia peke yake vita na hali ya usalama nchini Uganda baada ya ushindi. Jambo hilo lilizidi kudidimiza nchi katika ufukara na kufelisha mipango yake ya maendeleo. Tanzania ilimaliza kutoka katika hali hiyo mwaka 2007 tu, Uganda ilipolipa madeni yake.

  • Mambo, Andrew; Julian, Schofield (2007). "Military Diversion in the 1978 Uganda-Tanzania War". Journal of Political and Military Sociology. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Novemba 2011. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita vya Kagera kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.