Wilaya ya Tunduru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Tunduru (kijani) katika mkoa wa Ruvuma.

Wilaya ya Tunduru ni wilaya mojawapo katika Mkoa wa Ruvuma. Kwa upande wa kusini Tunduru inapakana na Msumbiji, upande wa magharibi na wilaya ya Namtumbo, kaskazini na mkoa wa Lindi na upande wa mashariki na Mkoa wa Mtwara.

Wakazi walio wengi ni Wayao.

Wilaya ina tarafa 7 ambazo ni Mlingoti, Nalasi, Nakapanya, Nampungu, Matemanga, Lukumbule, Namasakata na Mbesa kwa Tunduru mjini.

Tunduru kuna chuo cha Biblia cha Kanisa la Biblia Tanzania katika kiungo cha Nanjoka. Shule za sekondari ni Tunduru Sekondari, Mataka, Frank Weston na Masonya,

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 247,976 [1].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Tunduru - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chiwana | Jakika | Kalulu | Kidodoma | Ligoma | Ligunga | Lukumbule | Majengo | Majimaji | Marumba | Masonya | Matemanga | Mbati | Mbesa | Mchangani | Mchesi | Mchoteka | Mchuluka | Mindu | Misechela | Mlingoti Magharibi | Mlingoti Mashariki | Mtina | Muhuwesi | Nakapanya | Nakayaya | Nalasi Magharibi | Nalasi Mashariki | Namakambale | Namasakata | Namiungo | Nampungu | Namwinyu | Nandembo | Nanjoka | Ngapa | Sisikwasisi | Tinginya | Tuwemacho


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Tunduru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.