Wilaya ya Mkinga
Wilaya ya Mkinga ni wilaya moja ya Mkoa wa Tanga iliyopo ufukoni wa Bahari Hindi. Ilianzishwa rasmi mwaka 2005 baada ya kugawanywa kutoka Wilaya ya Muheza. Makao makuu ya wilaya yapo Kasera.
Idadi ya wakazi ilikuwa mnamo watu 118,065 [1] wanaoishi katika tarafa 2, ambazo ni Maramba na Mkinga, kata 21 na vijiji 85.[2]
Wilaya imepakana na Wilaya ya Muheza na Tanga kwa upande wa kusini, Wilaya ya Lushoto na Korogwe upande wa magharibi, Kenya upande wa kaskazini na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki.
Maeneo ya wilaya hii ni kilomita za mraba 2,948.
Uchumi wa Mkinga[hariri | hariri chanzo]
Shughuli kuu za wakazi wake ni kilimo, ufugaji, biashara, uzalishaji wa chumvi na uvuvi. Asilimia 85% ya eneo la Wilaya ya Mkinga yaani 2505.8 km² linafaa kwa kilimo na ufugaji.
Zao la korosho ni zao kuu la biashara. Mashamba darasa ya zao la mikorosho yameanzishwa katika vijiji vya Mahandakini, Mavovo, Kwangena na Totovu. Katika kuendeleza zao la korosho, shamba la kutoa mbegu na vikonyo vya mikorosho limeanzishwa, Pia kuna mchakato wa kuanzisha bustani ya miche ya mikorosho.
Mnamo mwaka 2012 wilaya ilikuwa na ng’ombe 1,962 wa kisasa, ng’ombe 29,990 wa kiasili, mbuzi 27,864, kuku 111,515, na kondoo 7,055.[3]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mkinga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
![]() |
Kata za Wilaya ya Mkinga - Mkoa wa Tanga - Tanzania |
![]() |
---|---|---|
Boma | Bosha | Bwiti | Daluni | Doda | Duga | Gombero | Kigongoi Magharibi | Kigongoi Mashariki | Kwale | Manza | Mapatano | Maramba | Mayomboni | Mhinduro | Mkinga | Mnyenzani | Moa | Mtimbwani | Mwakijembe | Parungu Kasera | Sigaya |