Mayomboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mayomboni ni jina la kata ya Wilaya ya Mkinga katika Mkoa wa Tanga , Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 4,001 [1] waishio humo.

Mayomboni ni kata ya kaskazini-mashariki kabisa ya Tanzania ikiwa kwenye ufuko wa Bahari Hindi pale ambako mpaka wa Kenya na Tanzania inafika baharini. Zamani barabara kuu ya Mombasa - Tanga ilipita hapa na kuvuka mpaka kwenye kijiji cha Yasini. Wakati wa ukoloni wa Kijerumani kulikuwa hapa kituo cha forodha.

Kwenye Januari 1915 yalitokea hapa mapigano ya Yasini kati ya jeshi la Schutztruppe ya Kjerumani na jeshi la Kihindi-Kiingereza.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Tanga - Mkinga DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mayomboni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Kata za Wilaya ya Mkinga - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Boma | Bosha | Bwiti | Daluni | Doda | Duga | Gombero | Kigongoi Magharibi | Kigongoi Mashariki | Kwale | Manza | Mapatano | Maramba | Mayomboni | Mhinduro | Mkinga | Mnyenzani | Moa | Mtimbwani | Mwakijembe | Parungu Kasera | Sigaya