Nenda kwa yaliyomo

Mwakijembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mwakijembe ni kata ya Wilaya ya Mkinga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania. Msimbo wa posta ni 21521.

Ni kata yenye vijiji vinne, yaani Mkota, Mbuta, Perani na Mwakijembe ambacho ni kijiji kilichozaa jina la kata hii.

Imepakana na kata za Daluni, Duga, Parungu Kasera na upande mwingine imepakana na nchi ya Kenya.

Kata ina neema ya kupitiwa na mto Umba.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,708 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,515 [2] waishio humo.

Wakazi wa kata hii ni Wamasai, Waduruma, Wakamba na Wataita.

Shughuli kubwa zinazofanywa katika kata hii ni kuuza mkaa na kuchimba madini.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Tanga - Mkinga DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
Kata za Wilaya ya Mkinga - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Boma | Bosha | Bwiti | Daluni | Doda | Duga | Gombero | Kigongoi Magharibi | Kigongoi Mashariki | Kwale | Manza | Mapatano | Maramba | Mayomboni | Mhinduro | Mkinga | Mnyenzani | Moa | Mtimbwani | Mwakijembe | Parungu Kasera | Sigaya


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mwakijembe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.