Wilaya ya Missenyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wilaya ya Misenyi ni wilaya moja ya Mkoa wa Kagera yenye postikodi namba 35300 [1]. Ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Bukoba Vijijini. Wilaya hii imepakana na Uganda upande wa kaskazini, Ziwa Viktoria upande wa mashariki na Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera uko upande wa kusini. Eneo la wilaya liko upande wa magharibi ya Ziwa Viktoria.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 202,632 [2]

Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi (Missenyi District Council) ni moja kati ya serikali 8 za kiwilaya kwenye Mkoa wa Kagera. Eneo la wilaya ni 2709 km².

Maeneo ya wilaya hupokea mvua mara mbili kwa mwaka; Kwenye mwambao wa Ziwa Viktoria mvua hufikia hadi milimita 1,400 na 2,000 kwa mwaka, kwenye nyansa za juu kati ya 1,000 na 1,400 mm; upande wa magharibi kiwango hushuka hadi 600 na 1,000 mm kwa mwaka.

Marejeo

Viungo vya Nje


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Missenyi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.


Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bugika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga