Minziro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Minziro ni jina la kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35315 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,951 waishio humo.[2]

Kata hii ipo mpakani kabisa mwa Uganda na ipo katikati ya msitu.

Lugha zinazotumika Minziro ni Kihaya, Kiganda na Kiswahili. Kutokana na kutumika kwa kiwango kikubwa na wakazi wa Minziro, Kiganda ni kama lugha mama ya wengi.

Kata inaundwa na vijiji vitatu, ambavyo ni Kigazi, Minziro na Karagala.

Wananchi wanategemea kilimo cha kahawa kama zao la biashara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Minziro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.