Nsunga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nsunga ni jina la kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35316 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,001 waishio humo.[2]

Baadhi ya vijiji katika kata hii ni pamoja na:

  • Igayaza
  • Ngando
  • Omurugando
  • Byamutemba

Watu wanaoishi katika kata hii wanajihusisha na kilimo cha kahawa, ndizi, mboga mboga, na ufugaji. Nsunga ni kata inayokua kwa kasi, na uchumi wake unaotegemea kilimo unakwamua watu wengi katika umaskini. Ni kata ambamo ndani yake kuna kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar, ambapo wakazi wa kata hii pia hujihusisha na kilimo cha miwa.

Kata hii pia imekuwa na umaarufu kwa kuwa na ukanda wenye kutuama maji, ambapo nyakati za kiangazi hutumika katika kuzalisha mboga za majani na matunda. Maeneo haya ni pamoja na Kyarukorongo, Kigwanga na Gelegele, ambako mboga nyingi huzalishwa, na hasa katika mkoa wa Kagera. Wakulima hawa hutegemea soko kuu la Bunazi, lililoko wilaya ya Missenyi.

Kata hii pia ina milima mingi ambayo ilitumika kwa umuhimu zaidi katika vita vya Kagera (1978-1979).

Tarehe 10 Septemba 2016 Nsunga ilikuwa mahali pa kitovu cha tetemeko la ardhi la Kagera 2016.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nsunga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.