Ruzinga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ruzinga ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35305 [1].

Kata ya Ruzinga iko kilomita 52 kaskazini Magharibi mwa mji wa Bukoba. Ukielekea barabara ya kwenda Uganda, ukifika sehemu inayoitwa Amshenyi kilomita 24 unapinda kuelekea kaskazini, barabara inakoishia ndiko kata Ruzinga iliko. Iko umbali wa kilomita 60 kutoka makao makuu ya wilaya.

Ruzinga ni kata yenye vijiji viwili ambavyo ni: Mugongo na Ruhija. Ina vitongoji tisa. Ruhija ina vitongoji vinne na Mugongo ina vitongoji vitano. Vitongoji vya Ruhija ni Kaaro, Busimba, Busheza na Katano. Vya Mugongo ni Katunga, Kaina, Ilundu, Mugongo na Kalegeya.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 3,280 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,293 waishio humo, wakiwemo wanaume 1,549 na wanawake 1,744. [3]

Kata hii ina shule tatu za msingi na shule moja ya sekondari. Shule hizo ni shule ya msingi Ruzinga, Shule ya msingi Ruhija, Shule ya msingi Mugongo na Shule ya sekondari Ruzinga.

Kata Ruzinga ni eneo lililozungukwa na tingatinga mfano wa kisiwa kuna barabara moja inayoingia na kutoka. Ni eneo lenye watu wengi waliopata elimu rasmi ukizingatia kwamba shule ya msingi Ruzinga imekuwepo zaidi ya miaka 80 iliyopita.

Ina ardhi yenye rutuba kwa kustawisha mazao ya kahawa, migomba, vanila, miti ya mbao na matunda, mihogo, viazi na bustani za mbogamboga. Hupata mvua karibu mwaka mzima.

Wakazi wa Ruzinga kuanzia mwaka 2005 wamekuwa na tamasha la kuhamasishana kuchangia maendeleo ya kata. Tamasha hili linafanyika kila tarehe 31/12 na huwaunganisha Wanaruzinga wanaoishi ndani na nje ya Ruzinga.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 177
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ruzinga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.