Kyaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kyaka ni jina la kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35312 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,190 waishio humo.[2]

Kyaka iko upande wa kusini wa mto Kagera. Kutoka hapa kuna faraja linalounganisha sehemu ya mkoa upanda wa kaskazini ya mto Kagera. Wakati wa vita ya Kagera jeshi la Uganda likavamia maeneo upande wa askazini ya mto wakajaribu kuvunja daraja la Kayaka kwa mabomu ya ndege za vita. Hii ilishindikana kwa hiyo wataalamu kutoka migodi ya Kilembe walifaulu kubomoa daraja kwa kutumia baruti kali mwanzo wa Novemba 1978[3]. Daraja likajengwa upya baada ya vita.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
  3. Nyerere and Africa: End of an Era. New Africa Press (2010). Iliwekwa mnamo 16 March 2013.
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyaka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.