Kassambya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kassambya ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35314 [1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 37,028 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 26,633 waishio humo.[3]

Ni kata inayoundwa na vijiji sita ambavyo ni: Kassambya, Bunazi, Mabuye, Nyabihanga, Gabulanga na Kakindo.

Ina shule za sekondari 2 ambazo ni Shule ya sekondari Bunazi na Shule ya sekondari Gabulanga, pia kila kijiji kina shule ya msingi, hivyo basi shule za msingi ziko sita.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 177
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kassambya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.