Mkoa wa Unguja Kusini


Mkoa wa Unguja Kusini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Uko kwenye kisiwa cha Unguja ambacho ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Unapakana na mikoa yote miwili mingine ya kisiwa hicho: Mkoa wa Unguja Kaskazini na Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi mbali ya Bahari Hindi. Eneo la mkoa ni km² 854 likiwa na wakazi 195,873 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 (115,588 mwaka 2012) wanaoishi katika wilaya mbili ikiwa Wilaya ya Kati yenye wakazi 132,717 (73,346 mwaka 2012) na Wilaya ya Kusini ina wakazi 63,156 (39,242 mwaka 2012) [1].
Makao makuu yako Koani.
Msimbo wa posta ni namba 72000.
Wakazi wa eneo hili la kisiwa cha Unguja, mbali na kujishughulisha na uvuvi kwenye Bahari ya Hindi, ni maarufu pia kwa kilimo cha zao la karafuu, zao linalofanya Zanzibar kujulikana zaidi kama kisiwa cha viungo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Unguja Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
