Nenda kwa yaliyomo

Mtwara (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Manisipaa ya Mtwara)


Mtwara
Mtwara is located in Tanzania
Mtwara
Mtwara

Mahali pa mji wa Mtwara katika Tanzania

Majiranukta: 10°16′12″S 40°11′24″E / 10.27000°S 40.19000°E / -10.27000; 40.19000
Nchi Tanzania
Mkoa Mtwara
Wilaya Mtwara Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 146,772
Sehemu ya magharibi mwa Bahari ya Hindi kama inavyoonekana kutoka Mtwara.

Mtwara ni mji wa Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mtwara wenye postikodi namba 63100.

Mtwara ni mji wa bandari kando ya Bahari Hindi karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

Kiutawala Mtwara ni wilaya ya Mtwara mjini, umeunganishwa pamoja na mji wa kihistoria wa Mikindani katika halmashauri ya manisipaa.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 146,772 [1]. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilikuwa 92,602 [2] .

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mtwara ni mji mpya ulioanzishwa tangu 1947 mahali ambako kulikuwa na kijiji kidogo cha wavuvi tu. Waingereza waliotawala Tanganyika wakati ule walipanga mradi mkubwa wa kilimo katika Tanganyika ya Kusini wakahitaji bandari kwa ajili ya kubeba mazao yake. Mji ulipangwa kitaalamu kwa ajili ya wakazi 200,000 na mahali palichaguliwa kwa sababu ya bandari asilia iliyofaa hata kwa meli kubwa.

Bandari ilijengwa na mji mpya ulianzishwa lakini tangu 1950 ilionekana ya kwamba mradi wa kilimo kilishindikana. Mwaka 1953 mji ulikuwa na wakazi 36,999 pekee. Mji haukuendelea, ukarudi nyuma hasa kwa sababu pwani ya Kusini ilikosa barabara na njia za mawasiliano. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji ilizuia biashara ya mpakani.

Tangu miaka ya 1990 uchumi ulianza kusonga mbele polepole. Barabara ya lami inaendelea kutengenezwa kutoka Dar es Salaam kuelekea Mtwara. Tangu kukamilishwa kwa daraja la mto Rufiji mawasiliano kwa barabara yameboreshwa hata wakati wa mvua. Vilevile feri inayovuka mto Ruvuma imeongeza biashara ya mpakani na Msumbiji.

Mawasiliano

[hariri | hariri chanzo]

Mtwara ni kitovu cha usafiri katika kusini-mashariki ya Tanzania. Mabasi kadhaa hufika kila siku kutoka Dar es Salaam. Meli hufika mara kwa mara. Uwanja wa ndege hufikiwa na Air Tanzania mara tano kwa wiki. Barabara ya lami imefikia Lindi na Masasi. Feri ya mto Ruvuma inabeba magari na mizigo karibu kila siku. Daraja kwenda Msumbiji unapangwa.

Kuna pia mipango ya kujenga barabara imara ya lami kutoka Mtwara kwenda Songea na Ziwa Nyasa itakayowezesha bandari ya mji kuhudumia kusini mwote mwa Tanzania pamoja na Malawi.

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Tanzania.go.tz/census/districts/mtwaraurban". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-05-03. Iliwekwa mnamo 2003-05-03. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
Kata za Wilaya ya Mtwara Mjini - Tanzania

Chikongola | Chuno | Jangwani | Kisungule | Likombe | Magengeni | Magomeni | Majengo | Mitengo | Mtawanya | Mtonya | Naliendele | Rahaleo | Reli | Shangani | Tandika | Ufukoni | Vigaeni


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mtwara (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.