Mkoa wa Unguja Kaskazini
Mkoa wa Unguja Kaskazini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 73000. Uko Unguja ambayo ni kisiwa kikubwa cha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Makao makuu ya mkoa yako Mkokotoni.
Kuna wilaya mbili ambazo ni Kaskazini Unguja 'A' (105,780 mwaka 2012 na 157,369 mwaka 2022) na Kaskazini Unguja 'B' (81,675 mwaka 2012 na 99,921 mwaka 2022)[1][2].
Eneo la mkoa ni km² 470 ambako kuna jumla ya wakazi 257,290 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022[3].
Wengi wanajishughulisha na uvuvi na kilimo. Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna kilimo cha karafuu.
Upande wa magharibi utalii umeanza kuwa muhimu. Eneo la Ras Nungwi ni sehemu moja yenye mahoteli ya watalii wa nje.
Kisiwa cha Tumbatu ni sehemu ya mkoa huu.
Miji ya mkoa ndiyo Mkokotoni, Mahonda na Gamba.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2018-01-10.
- ↑ https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Census2022/Administrative_units_Population_Distribution_Report_Tanzania_volume1a.pdf
- ↑ https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Census2022/Administrative_units_Population_Distribution_Report_Tanzania_volume1a.pdf
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Dira mikoani: Kaskazini Unguja Archived 8 Mei 2006 at the Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Unguja Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |