Nachingwea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Nachingwea (kijani) katika mkoa wa Lindi.

Wilaya ya Nachingwea ni kati ya wilaya moja za Mkoa wa Lindi yenye postikodi namba 65110[1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 162,081 [1].

Wilaya hii imepakana na wilaya za Ruangwa upande wa kaskazini Lindi Vijijini upande wa mashariki halafu na mikoa ya Mtwara na Ruvuma upande wa kusini.

Nachingwea kuna hospitali, Chuo cha Ualimu, shule za sekondari 3 na za msingi 81 wilayani.

Eneo hili lilikuwa sehemu ya mradi wa karanga wakati wa ukoloni wa Uingereza.

Kuna madini ya nikeli katika Nachingwea na kampuni ya IMX Resources NL (zamani Goldstream Mining) kutoka Australia imeanzisha kampuni "Continental Nickel" ya kuchimba nikeli hii lakini 2008 bado imetafuta pesa kwenye soko la hisa ya Kanada.


Asili ya Nachingwea[hariri | hariri chanzo]

Neno Nachingwea asili yake imetokana na mti mmoja uliokuwa ukiitwa Ngwea. Wakazi wa makao makuu ya wilaya ya Nachingwea wakati huo Ruponda walikuwa wakienda kuchota maji chingi ya mti wa Ngwea, kwa hiyo walikuwa wakisema Nachi Ngwea wakimaanisha naenda kwenye Ngwea, yaani maana yake nakwenda kuchota maji kwenye ngwea, ndipo jina hilo Nachingwea likashika kasi na kuwa Nachingwea ya leo. Makao makuu ya mwanzo ya Nachingwea yalikuwa Ruponda.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Picha za Nachingwea kwa Flikr [www.minebox.com/story.asp?articleId=8937 ]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Nachingwea - Mkoa wa Lindi - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Boma | Chiola | Chiumbati Shuleni | Kiegei | Kilimani Hewa | Kilimarondo | Kipara Mnero | Kipara Mtua | Lionja | Marambo | Matekwe | Mbondo | Mchonda | Mitumbati | Mkoka | Mkotokuyana | Mnero Miembeni | Mnero Ngongo | Mpiruka | Mutua | Nachingwea Mjini | Naipanga | Naipingo | Namapwia | Namatula | Nambambo | Namikango | Nang'ondo | Nangowe | Nditi | Ndomoni | Ngunichile | Raha leo | Ruponda | Stesheni | Ugawaji