Wilaya ya Tarime

Wilaya ya Tarime ni wilaya mojawapo ya wilaya za Mkoa wa Mara. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 339,693[1]. Misimbo ya posta katika wilaya hii inaanza kwa 314.
Zamani ilijulikana kwa jina la "Wilaya ya Mara Kaskazini". Mwaka 2006 sehemu ya mashariki ya Tarime imekuwa wilaya mpya ya Rorya lakini haina makao makuu bado.
Tarime imepakana na Kenya (wilaya za Migori, Trans Mara na Kisii) upande wa kazkazini na mashariki. Hifadhi ya wanyama ya Masai Mara ya Kenya uko upande wa mashariki pia. Upande wa kusini umepakana na wilaya za Musoma mjini, Musoma vijijini na wilaya ya Serengeti. Upande wa magharibi iko wilaya mpya ya Rorya.
Makao makuu ya wilaya yapo mjini Tarime.
Wakazi[hariri | hariri chanzo]
Tarime ni eneo la Wakuria hasa waliopo pia ng'ambo ya mpaka nchini Kenya. Wakazi asilia wengine ni Wasimbiti.
Wakazi wengi ni wakulima na wafugaji wa wanyama kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo. Eneo la Tarime linajulikana kwa matatizo ya mapigano ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.
Migodi ya dhahabu[hariri | hariri chanzo]
Karibu na kijiji cha Nyamongo katika kata ya Nyamwaga kuna migodi ya dhahabu ya North Mara Gold Mine inayomilikiwa na kampuni Acacia Mining kutoka Uingereza. Kuwepo kandokando kwa utajiri wa dhahabu na umaskini ya wenyeji kunasababisha mara kwa mara kuningia kwa wanavijiji katika eneo la migodi wanapojaribu kukusanya mtapo mwenye dhahabu.
Mwaka 2011 na 2013 wanavijiji kadhaa walioingia katika eneo la migodi waliuawa na maafisa wa polisi waliosaidia walinzi wa kampuni[2][3]. Shirika za haki za binadamu walishtaki kampuni kwa niaba ya wahanga mbele ya mahakama huko Uingereza. Kesi zilisimamishwa mwezi wa Fevruari 2015 baada ya kampuni kulipa fidia kwa familia husika.[4][5]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Sensa ya 2012, Mara - Tarime-District-Council
- ↑ http://www.bloomberg.com/news/articles/2010-12-23/shooting-gold-diggers-at-african-mine-seen-amid-record-prices Shooting Gold Diggers at African Mine Seen Amid Record Prices, Bloomberg.com December 23, 2010
- ↑ http://www.facing-finance.org/en/database/cases/violence-at-north-mara-goldminegewalt-und-vertreibung-bei-der-goldmine-in-north-mara/ Archived 1 Novemba 2015 at the Wayback Machine. Barrick Gold: Human Rights Violations in Tanzania, Facing Finance database
- ↑ http://business-humanrights.org/en/african-barrick-gold-lawsuit-re-tanzania African Barrick Gold lawsuit (re Tanzania) Business & Human Rights Resource Center
- ↑ http://www.theguardian.com/environment/2015/feb/10/british-gold-mining-settlement-deaths-tanzanian-villagers British gold mining firm agrees settlement over deaths of Tanzanian villagers Guardian newspaper (UK) Tuesday 10 February 2015
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
Filamu juu ya matata na mapigano wakati wa kempeni ya uchaguzi 2009 Tarime Archived 4 Oktoba 2010 at the Wayback Machine.
![]() |
Kata za Wilaya ya Tarime - Mkoa wa Mara - Tanzania |
![]() | ||
---|---|---|---|---|
Binagi * Bomani * Bumera * Genyange * Gorong'a * Itiryo * Kemambo * Kentare * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Manga (Tarime) * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nkende * Nyakonga * Nyamaranga * Nyamisangura * Nyamwaga * Nyandoto * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Sabasaba * Sirari * Susuni * Turwa
|