Matongo (Tarime)
Matongo ni kata ya Wilaya ya Tarime katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31412 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,176 waishio humo.[2]
Kata ya Matongo inaundwa na vijiji vinne: Mjini Kati, Nyangoto, Nyabichune na Matongo.
Umbali kutoka Tarime Mjini hadi Matongo ni kilometa 30.
Shughuli kubwa za kiuchumi ni uchimbaji wa madini, ufugaji na kilimo.
Maeneo ya kata hii ndiyo sehemu pekee katika wilaya ya Tarime ambapo madini ya dhahabu hupatikana kwa wingi. Mgodi wa Kampuni ya Acacia, North Mara, upo ndani ya kata hii.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Kata za Wilaya ya Tarime - Mkoa wa Mara - Tanzania |
![]() | ||
---|---|---|---|---|
Binagi * Bomani * Bumera * Genyange * Gorong'a * Itiryo * Kemambo * Kentare * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Manga (Tarime) * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nkende * Nyakonga * Nyamaranga * Nyamisangura * Nyamwaga * Nyandoto * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Sabasaba * Sirari * Susuni * Turwa
|