Wilaya ya Rorya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rorya ni wilaya mpya katika mkoa wa Mara yenye postikodi namba 31300[1]. Hadi mwaka 2006 ilikuwa sehemu ya magharibi ya wilaya ya Tarime. Makao makuu ya Wilaya ya Rorya ni Ingri Juu (31311 Mirare).

Eneo la wilaya liko kati ya ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi na Tarime upandwe wa mashariki. Upande wa kaskazini inapakana na nchi ya Kenya na upande wa kusini na wilaya ya Musoma.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi wapatao 265,241 waishio humo. [2]

Walio wengi ni Waluo. Makabila mengine ni Wakine, Wakurya, Wasimbiti, Wahacha, Wasweta na mengineyo. Hii ndiyo wilaya yenye makabila mengi zaidi nchini Tanzania.

Taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Rorya kuanzia mwaka 2015

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Rorya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Rorya - Mkoa wa Mara - Tanzania
Flag of Tanzania.svg

Bukura * Bukwe * Goribe * Ikoma * Kigunga * Kirogo * Kisumwa * Kitembe * Komuge * Koryo * Kyang'ombe * Mirare * Mkoma * Nyahongo * Nyamagaro * Nyamtinga * Nyamunga * Nyathorogo * Rabour * Roche * Tai