Nenda kwa yaliyomo

Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Misimbo ya posta)
Mfano wa matumizi ya Msimbo wa Posta katika anwani ya barua (alama nyekundu)

Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.

Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.

Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.

Muundo wa tarakimu katika msimbo wa posta wa Tanzania

Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:

  • tarakimu ya kwanza inaonyesha kanda
  • tarakimu ya pili (pamoja na inayotangulia) inaonyesha mkoa
  • tarakimu ya tatu (pamoja na zinazotangulia) inaonyesha wilaya au halmashauri
  • tarakimu za nne na tano (pamoja na zinazotangulia) zinaonyesha kata.
    • Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
    • Hakuna misimbo ya pekee kwa kata zote za Tanzania; wakati mwingine kata kadhaa za wilaya ileile zimeunganishwa kwa kazi ya posta na kuwa na msimbo mmoja[1]

Mfano:

6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko.
6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani
6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi
6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa (651 ni Lindi mjini, 563 Nachingwea, 655 Liwale, na kadhalika)
• Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.

Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 (Kilwa Masoko) hadi 6 5 4 2 1 (Kibata).

Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya „65421 Kibata“ inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani („6“) na Mkoa wa Lindi („65“). Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.

Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.

Kanda

Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:

  1. Dar es Salaam (Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Kigamboni)
  2. Kaskazini
  3. Ziwa
  4. Kati
  5. Nyanda za Juu Kusini
  6. Pwani
  7. Zanzibar

Ugawaji wa misimbo ya posta kwenye mikoa na wilaya

1. Kanda ya Dar es Salaam

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Dar es Salaam11
Manisipaa ya Ilala11, 12Kivukoni 11101
Manisipaa ya Kinondoni14Magomeni 14101
Manisipaa ya Temeke15Temeke 15101
Manisipaa ya Ubungo16Mburahati 16101
Manisipaa ya Kigamboni17Kimbiji 17101

2. Kanda ya Kazkazini

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Tanga21
Mji wa Tanga211,

212

Central 21101

Tangasisi 21201

Wilaya ya Pangani213Bushiri 21307
Wilaya ya Muheza214Majengo 21401
Wilaya ya Mkinga215Daluni 21501
Mji wa Korogwe216Manundu 21601
Wilaya ya Korogwe216Mashewa 21627
Wilaya ya Lushoto217Sunga 21723
Wilaya ya Handeni218Kabuku 21815
Mji wa Handeni218Chanika 21801
Wilaya ya Kilindi219Songe 21901
Mkoa wa Arusha23
Mji wa Arusha231Sekei 23101
Wilaya ya Arusha232Olturumet 23201
Wilaya ya Meru233Usa River 23301
Wilaya ya Monduli234Monduli Mjini 23401
Wilaya ya Longido235Longido 23501
Wilaya ya Karatu236Karatu 23601
Wilaya ya Ngorongoro237Orgosorok 23701
Mkoa wa Kilimanjaro25
Manisipaa ya Moshi251Mawenzi 25101
Wilaya ya Moshi252Mabogini 25201
Wilaya ya Siha254
Wilaya ya Hai253Machame Mashariki 25301
Wilaya ya Mwanga255Jipe 25501
Wilaya ya Same256Same 25601
Wilaya ya Rombo257Mahida 25701
Mkoa wa Manyara27
Mji wa Babati271Babati 27101
Wilaya ya Babati272Magugu 27201
Wilaya ya Hanang273Katesh 27301
Wilaya ya Mbulu274Ayomohe 27401
Wilaya ya Kiteto275Kibaya 27501
Wilaya ya Simanjiro276Orkesumet 27601

3. Kanda ya Ziwa

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Geita30
Wilaya ya Geita301Kalangalala 30101
Wilaya ya Nyang'hwale302Nyang'hwale 30201
Wilaya ya Chato303Chato 30301
Wilaya ya Mbogwe304Iponya 30401
Wilaya ya Bukombe305Bukombe 30501
Mkoa wa Mara31
Manisipaa ya Musoma311Mwigobero 31102
Wilaya ya Musoma312Murangi 31217
Wilaya ya Butiama312Makojo 31220
Wilaya ya Rorya313Bukura 31301
Wilaya ya Tarime314Bomani 31401
Wilaya ya Bunda315Bunda Mjini 31501
Wilaya ya Serengeti316Mugumu Mjini 31601
Mkoa wa Mwanza33
Manisipaa ya Nyamagana331Nyamagana 33101
Manisipaa ya Ilemela332Nyakato 33201
Wilaya ya Sengerema333Ibisabageni 33301
Wilaya ya Magu334Magu mjini 33401
Wilaya ya Misungwi335Nhundulu 33501
Wilaya ya Ukerewe336Nansio 33601
Wilaya ya Kwimba338Ngudu 33801
Mkoa wa Kagera35
Manisipaa ya Bukoba351Bakoba 35101
Wilaya ya Bukoba Vijijini352Buhendangabo 35201
Wilaya ya Missenyi353Ishozi 35301
Wilaya ya Karagwe354Kayanga 35402
Wilaya ya Muleba355Rushwa 35502
Wilaya ya Biharamulo356Biharamulo Mjini 35601
Wilaya ya Ngara357Ngara Mjini 35701
Wilaya ya Kyerwa358Kyerwa 35801
Mkoa wa Shinyanga37
Manisipaa ya Shinyanga371
Wilaya ya Shinyanga Vijijini372
Wilaya ya Kahama37337311 Bugarama
Mji wa Kahama373Majengo 37301
Wilaya ya Kishapu375Kishapu 37501
Mkoa wa Simiyu39
Wilaya ya Bariadi391Bariadi 39101
Wilaya ya Itilima392Lagangabilili 39201
Wilaya ya Maswa393BuchambiI 39301
Wilaya ya Meatu394Lubiga 39401
Wilaya ya Busega395Kabita 39501

4. Kanda ya Kati

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Dodoma41
Manisipaa ya Dodoma411 ,

412

Tambukareli  41104 

Makutopora 41201

Wilaya ya Bahi413Bahi 41301 Bahi Sokoni
Wilaya ya Chamwino414Chilonwa 41401
Wilaya ya Kongwa415Kongwa 41501
Wilaya ya Mpwapwa416Mpwapwa mjini 41601
Wilaya ya Kondoa417Kondoa mjini 41701
Wilaya ya Chemba418Chemba 41801
Mkoa wa Singida43
Manisipaa ya Singida431
Wilaya ya Singida Vijijini432
Wilaya ya Iramba433Kiomboi 43301
Wilaya ya Manyoni434Manyoni Urban 43401
Wilaya ya Mkalama435Kinyangiri 43501
Wilaya ya Ikungi436Ihanja 43601
Mkoa wa Tabora45
Manisipaa ya Tabora451
Wilaya ya Uyui452Goweko 45201
Wilaya ya Sikonge453Sikonge 45301
Wilaya ya Nzega454Nzega mjini 45401
Wilaya ya Urambo455Urambo 45501
Wilaya ya Igunga456Igunga 45601
Wilaya ya Kaliua457Kaliua 45701
Mkoa wa Kigoma47
Manisipaa ya Kigoma-Ujiji471
Wilaya ya Kigoma Vijijini472
Mji wa Kasulu473
Wilaya ya Kasulu473Kasulu Mjini 47301
Wilaya ya Kibondo474Kibondo Mjini 47401
Wilaya ya Buhigwe475Buhigwe 47501
Wilaya ya Uvinza476Uvinza 47601
Wilaya ya Kakonko477Nyabibuye  47709 

5. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Katavi50
Mji wa Mpanda501
Wilaya ya Tanganyika502Ikola  50203 
Wilaya ya Mlele503Inyonga 50301
Mkoa wa Iringa51
Manisipaa ya Iringa511
Wilaya ya Iringa Vijijini512
Wilaya ya Kilolo513Irole 51301
Mji wa Mafinga514Boma/Mafinga 51401
Wilaya ya Mufindi514
Mkoa wa Mbeya53
Mji wa Mbeya531
Wilaya ya Mbeya Vijijini532
Wilaya ya Rungwe535Bulyaga 53501
Wilaya ya Mbarali536Rujewa 53601
Wilaya ya Kyela537Kyela mjini 53701
Wilaya ya Chunya538
Mkoa wa Songwe54
Wilaya ya Songwe541
Wilaya ya Mbozi542
Wilaya ya Ileje543
Wilaya ya Momba544
Mji wa Tunduma544
Mkoa wa Rukwa55
Manisipaa ya Sumbawanga551Izia  55102 
Wilaya ya Sumbawanga Vijijini552
Wilaya ya Nkasi553Namanyere 55301
Wilaya ya Kalambo554Matai 55401
Mkoa wa Ruvuma57
Manisipaa ya Songea571Misufini  57102 
Wilaya ya Songea Vijijini572
Wilaya ya Namtumbo573Namtumbo 57301
Wilaya ya Mbinga574Mbinga Mjini 57401
Wilaya ya Nyasa575Mbambabay 57501
Wilaya ya Tunduru576
Mkoa wa Njombe59
Mji wa Njombe591Njombe Mjini 59101
Wilaya ya Njombe Vijijini592
Mji wa Makambako592
Wilaya ya Wanging'ombe593Mdandu 59301
Wilaya ya Ludewa594Ludewa 59401
Wilaya ya Makete595Iwawa 59501

6. Kanda ya Pwani

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Pwani61
Mji wa Kibaha611Mailimoja 61102
Wilaya ya Kibaha612Mlandizi 61201
Wilaya ya Bagamoyo613Yombo 61306
Wilaya ya Kisarawe614
Wilaya ya Mkuranga615Kiparang'anda 61502
Wilaya ya Rufiji
Wilaya ya Kibiti
616Utete 61601
Kibiti 61610
Wilaya ya Mafia617
Mkoa wa Mtwara63
Manisipaa ya Mtwara631
Wilaya ya Mtwara632
Wilaya ya Tandahimba633
Wilaya ya Newala634
Wilaya ya Masasi635Mwenge Mtapika 63529
Wilaya ya Nanyumbu636Nangomba  63601 
Mkoa wa Lindi65
Manisipaa ya Lindi651Makonde 65101
Wilaya ya Lindi652Nachunyu 65201
Wilaya ya Nachingwea653
Wilaya ya Kilwa654Kilwa Masoko 65401
Wilaya ya Liwale655Liwale Mjini 65501
Wilaya ya Ruangwa656Ruangwa 65601
Mkoa wa Morogoro67
Manisipaa ya Morogoro671
Wilaya ya Morogoro672
Wilaya ya Mvomero673
Wilaya ya Kilosa674
Wilaya ya Kilombero675
Wilaya ya Ulanga676Mahenge 67601
Wilaya ya Gairo677Gairo 67701

7. Kanda ya Zanzibar

EneoTarakimuMfano wa msimbo wa kata
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja71
Wilaya ya Mjini711
Wilaya ya Magharibi Unguja712Mwanakwerekwe 71201
Mkoa wa Kusini Unguja72
Wilaya ya Kusini721
Wilaya ya Kati722Dunga 72201
Mkoa wa Kaskazini Unguja73
Wilaya ya Kaskazini A731
Wilaya ya Kaskazini B732Mahonda 73201
Mkoa wa Kusini Pemba74
Wilaya ya Mkoani741
Wilaya ya Chake Chake742Chanjaani 74201
Mkoa wa Kaskazini Pemba75
Wilaya ya Wete751
Wilaya ya Micheweni752Micheweni 75201

Tanbihi

  1. Kwa mfano wilaya za Handeni mjini na vijijini ziko pamoja chini ya na. 218; ilhali kila kata ya wilaya ya Handeni vijijini ina msimbo wa posta, upande wa mjini kuna misimbo 3 pekee ilhali kata za mjini ziko 12.

Viungo vya Nje