Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Hai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Hai (kijani kilichokolea) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wilaya ya Hai ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Hai ilihesabiwa kuwa 210,533. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 240,999 [1].

Katika wilaya hiyo wakazi wengi ni Wachaga ambao huzungumza lahaja tofauti, kama Wamachame na Wamasama.

WIlaya hii ilitengwa mwaka 1975 kutoka Wilaya ya Moshi ya awali. Imepakana na Wilaya za Moshi Vijijini (mashariki), Arusha Vijiini na Siha (magharibi). Simanjiro (kusini), Rombo na Mbuga wa Kilimanjaro upande wa kaskazini.

Eneo lake ni kilomita za mraba 1,011. Kiutawala imegawiwa kwa tarafa 3 (Lyamungo, Machame na Masama), kata 14 na vijiji 60. Idadi ya vitongoji ni 248.

Kuna kanda 4 zenye tabianchi tofauti maana wilaya iko kenye mtelemko wa Mlima Kilimanjaro[2]

  • Kanda ya Kilele cha Mlima iko juu ya kimo cha mita 1,800 UB pamoja na kilele cha Kibo. Ni hasa maeneo ya mbuga na hifadhi ya taifa hivyo hakuna wakazi wa kudumu. Ni asilimia 27 za eneo la wilaya.
  • Kanda ya Juu: iko kwenye kimo kati ya mita 1,666 na 1,800 juu ya UB. Inafaa kwa kilimo cha kahawa na ndizi. Walio wengi ni wakulima wadogo wanaofuga pia ng'ombe wa maziwa na kuuza maziwa.
  • Kanda ya Kati: iko kwenye kimo kati ya mita 900 hadi 1,666 juu ya UB. Inapokea mvua kati ya milimita 700 hadi 1250 kwa mwaka; kilimo inafanana na kanda ya juu.
  • Kanda ya Chini iko kwenye kimo chini ya mita 900 juu ya UB. Hapa mvua inapungua hadi milimita 500-700 kwa mwaka. Mazao yanayostawi ni pamoja na maharagwe, mahindi, alizeti na mpunga. Ufugaji hapo chini si hasa ya maziwa ni zaidi ng'ombe wa kienyeji.
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Linganisha Investment Profile (taz. viungo vya Nje)
Ramani Wilaya au manisipaa Wakazi (2022) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro
Wilaya ya Hai 240,999 17 1,217
Wilaya ya Moshi Vijijini 535,803 32 1,300
Wilaya ya Moshi Mjini 331,733 21 63
Wilaya ya Mwanga 148,763 20 1,831
Wilaya ya Rombo 275,314 28 1,471
Wilaya ya Same 300,303 34 6,221
Wilaya ya Siha 139,019 17 1,217
Jumla 1,861,934 152 13,209
Wilaya ya Siha hii ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya wilaya ya Hai.
Marejeo: Mkoa wa Kilimanjaro
Kata za Wilaya ya Hai - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Bomang'ombe | Bondeni | KIA | Machame Kaskazini | Machame Magharibi | Machame Mashariki | Machame Narumu | Machame Uroki | Masama Kati | Masama Kusini | Masama Magharibi | Masama Mashariki | Masama Rundugai | Mnadani | Muungano | Romu | Weruweru


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Hai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.