Wilaya ya Kalambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Wilaya ya Kalambo
Wilaya ya Kalambo is located in Tanzania
Wilaya ya Kalambo
Wilaya ya Kalambo
Location in Tanzania
Majiranukta: 8°18′12″S 31°31′10″E / 8.30333°S 31.51944°E / -8.30333; 31.51944
Country Tanzania
Region Rukwa Region

Kalambo ni jina la wilaya mpya katika mkoa wa Rukwa yenye postikodi namba 55400[1], ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012.[2]

Makao makuu ya wilaya yako Matai.

Mkuu wa wilaya wa kwanza alikuwa Moshi Chang'a. [3]

Wilaya limepokea jina kutoka mto Kalambo unaopita hapa hadi kuishia kweye Maporomoko ya Kalambo upande wa Zambia.

Idadi ya wakazi wa wilaya ilikuwa 207,700 wakati wa sensa ya mwaka 2012. [4]

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Eneo la Kalambo liko kati ya Sumbawanga mjini na mpaka wa Zambia. Barabara ni chache na mbaya. Wakazi wengi hulima na kufuga. Mazao ya sokoni ni pamoja na mahindi, alizeti, maharagwa, muhogo na asali.[3] Watu wachache wanalima madini na kuvua samaki.[3]


Utawala[hariri | hariri chanzo]

Katika uchaguzi wa bunge la Tanzania Kalambo ni jimbo la uchguzi.[5]

Kata[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Kalambo huwa na kata 17:[6]

 • Kalambazite
 • Kasanga
 • Katazi
 • Katete
 • Kisumba
 • Legeza Mwendo
 • Mambwe Kenya
 • Mambwe Nkoswe
 • Matai

 • Mkali
 • Mkowe
 • Mnamba
 • Msanzi
 • Mwazye
 • Mwimbi
 • Sopa
 • Ulumi

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kalambo - Mkoa wa Rukwa - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Kasanga | Katazi | Katete | Kilesha | Kisumba | Legeza Mwendo | Mambwekenya | Matai | Mkali | Mkowe | Mnamba | Msanzi | Mwazye | Mwembenkoswe | Mwimbi | Sopa | Ulumi