Maporomoko ya Kalambo

Maporomoko ya Kalambo yanatokana na mto Kalambo ambao ni mpaka wa Tanzania na Zambia.
Maporomoko ya maji haya ukiachilia kuwa ni ya pili baada ya yale ya Tugela Afrika ya Kusini lakini pia ndiyo maporomoko pekee yanayogawa mpaka wa nchi mbili.
Maporomoko haya yapo katika kijiji cha Kapozwa Kata ya Kisumba, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa.
Maporomoko haya yamekuwa yakionekana na kutangazwa kuwa yapo Zambia na hivyo kuiondoa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye maporomoko yanayotambulika duniani.
Katika kijiji cha Kapozwa ambacho pia kilianzishwa kutokana na imani kuwa ukienda kuoga katika maporomoko hayo utapooza. Kwa kuambiwa hivyo wananchi wenyeji wa eneo hilo walipaita kijiji jina la kapozwa.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- Maporomoko ya kalambo
- Kalambo Archived 5 Machi 2010 at the Wayback Machine.
![]() | Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maporomoko ya Kalambo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |