Sopa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Sopa
Nchi Tanzania
Mkoa Rukwa
Wilaya Kalambo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 13,320

Sopa ni jina la kata ya Wilaya ya Kalambo katika Mkoa wa Rukwa, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,320 waishio humo.[1]

Utamaduni ya wakazi wa kata ya Sopa ni Wafipa wanaotumia lugha ya Kifipa katika mawasiliano.

Kata hii iliwahi kuwa sehemu ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini ikahamishwa kwenye wilaya mpya ya Kalambo mwaka 2012.

Kata ya Sopa ina jumla ya vijiji saba: Sopa, Mtuntumbe, Kasitu, Tatanda, Ilambila, Kalaela na Kamawe. Kuna jumla ya sekondari 2, ikiwemo Ulungu inapatikana kijiji cha Tatanda, pia shule ya sekondari Kanyele inapatikana kijiji cha Sopa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Sopa ni neno lililotokana na njia, njia ambayo Wajerumani walikuwa wakiitumia katika misafara yao; njia ilikuwa ikikatisha pembezoni mwa kijiji, ikitokea Lusaka, kupita Tatanda na kukatisha Sopa kuelekea Kasanga.

Njia hiyo iliweza kutumiwa na wakazi tofauti, awali ya yote kijiji kiliitwa Sote, baada ya kuzoeleka na wakazi au Wajerumani ndipo kijiji kikaitwa Sopa.

Baada ya mwaka 2002 hesabu ya sensa katika kijiji hicho ilifanyika na kuweza kupata idadi ya wakazi 18,141.

Kijiji hicho kilitawaliwa na viongozi tofauti akiwemo Alfredy Mwanga Sokoni.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sopa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kalambo - Mkoa wa Rukwa - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Kasanga | Katazi | Katete | Kilesha | Kisumba | Legeza Mwendo | Mambwekenya | Matai | Mkali | Mkowe | Mnamba | Msanzi | Mwazye | Mwembenkoswe | Mwimbi | Sopa | Ulumi