Wilaya ya Tanganyika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Tanganyika ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Katavi. Makao makuu ni Mpanda.

Hadi mwanzo wa mwaka 2016 wilaya hii ilijulikana kama "Wilaya ya Mpanda Vijijini" (Mpanda District Council). Jina latokana na Ziwa Tanganyika lililopo kwenye mpaka wa mashariki ya eneo hili.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 179,136.

Makao makuu ya wilaya yanajengwa katika kijiji cha Majalila kilichopo kwa sasa katika kata ya Tongwa. Uteuzi huu ulifuaza sifa za Majalila kufikika kwa urahisi kutokana na kuwa kandokando ya barabara kuu kutoka Mpanda - Kigoma, kuwepo kwa matenki mawili ya maji, na kuwa katika mpango wa kunufaika na umeme wa REA (Wakala wa umeme vijijini)[1]

Misimbo ya posta (postikodi)

Misimbo ya posta kwa kata za Wilaya ya Tanganyika ni:

  • Karema 50201
  • Kapalamsenga 50202
  • Ikola 50203
  • Katuma 50204
  • Sibwesa 50205
  • Mwese 50206
  • Kabungu 50207
  • Mpanda Ndogo 50208
  • Mishamo 50209
  • Kasekese 50211
  • Mnyagala 50212
  • Tongwe 50213
  • Ilangu 50214
  • Bulamata 50215
  • Ipwaga 50216

Angalia pia

Kuhusu asili ya jina "Tanganyika" ona hapa: Tanganyika_(ziwa)#Jina

Marejeo

  1. Kijiji cha Majalila sasa makao makuu rasmi ya Halmashauri ya Wilaya mpya ya Tanganyika, taarifa ya Issack Gerald kwenye tovuti ya p5tanzania.blogspot.com, iliangaliwa Juni 2017
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Tanganyika - Mkoa wa Katavi - Tanzania
Hadi 2016 wilaya hii ilijulikana kama Mpanda Vijijini
Flag of Tanzania.svg

Bulamata | Ikola | Ilangu | Ipwaga | Kabungu | Kapalamsenga | Karema | Kasekese | Katuma | Mishamo | Mnyagala | Mpandandogo | Mwese | Sibwesa | Tongwe