Nenda kwa yaliyomo

Gairo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Gairo
Nchi Tanzania
Mkoa Morogoro
Wilaya Gairo
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 12,295

Gairo ni makao makuu ya Wilaya ya Gairo katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67700.

Gairo uko kwenye barabara kuu ya Dodoma hadi Dar es Salaam na ni kituo cha kupitisha mizigo, pamoja na kituo cha kusafirisha mazao ya kilimo cha wilaya hiyo.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 12,684 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ya Gairo ilikuwa na wakazi wapatao 33,209, wengi wao wakiwa Wakaguru. [2] Kufikia 2002, idadi ya wakazi wa mji ilikuwa 16,982,[3]

Kikabila, watu wengi ni Wakaguru.

Maendeleo[hariri | hariri chanzo]

Gairo ni mmojawapo kati ya miji ambayo inakua sana nchini na unajulikana kwa kuwa unazalisha mazao ya biashara na chakula kama vile viazi vitamu, mahindi, maharagwe na vilevile kwa ufugaji.

Kutokana na ukaribu wake na barabara kuu ya Dodoma, mji wa Gairo umekuwa kati ya walishaji wakubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Hapo zamani Gairo ilikuwa chini ya jimbo la uchaguzi la Kilosa, baadaye ulipata kuwa jimbo linalojitegemea.

Mnamo Machi 2012 umefanywa wilaya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2015-03-22.
  3. "Gairo, Tanzania", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-07-16, iliwekwa mnamo 2023-05-14
Kata za Wilaya ya Gairo - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Chagongwe | Chakwale | Chanjale | Chigela | Gairo | Idibo | Italagwe | Iyogwe | Kibedya | Leshata | Madege | Magoweko | Mandege | Mkalama | Msingisi | Nongwe | Rubeho | Ukwamani


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gairo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.