Iyogwe
Iyogwe ni jina la kata ya Wilaya ya Gairo katika Mkoa wa Morogoro , Tanzania yenye Postikodi namba 67708. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 23,286 [1] waishio humo.
Wakazi walio wengi katika kijiji hiki ni kabila la Wakagulu na wachache ni Wanguu. Wakagulu walio wengi ni waumini wa dini ya kikristo na Wanguu walio wengi ni waumini wa dini ya kiislam.
Jina la Iyogwe lilitokana na mabishano ya Wakagulu wawali ambao walikuwa wakibishana kuhusu njia mwingine akisema "iyogweye" akiwa na maana 'hiyohiyo njia' lakini mwenzake alikuwa hakubaliani naye, hapo ndipo jina la Iyogwe lilipatikana mpaka leo.
Iyogwe ni kijiji ambacho kina sifa Wilaya ya Gairo kwa ujumla, hasa katika ulinzi na usalama wa jadi ujulikanao kama Uwu ama Umwano wa Ukaguru.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Sensa ya 2012, Morogoro - Gairo DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-21.
![]() |
Kata za Wilaya ya Gairo - Mkoa wa Morogoro - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Chagongwe | Chakwale | Chanjale | Gairo | Idibo | Iyogwe | Kibedya | Mandege | Msingisi | Nongwe | Rubeho | Chigela | Italagwe | Leshata | Madege | Magoweko | Mkalama | Ukwamani |