Nenda kwa yaliyomo

Kigoma-Ujiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Manisipaa ya Kigoma-Ujiji)


Kigoma Ujiji
Kigoma Ujiji is located in Tanzania
Kigoma Ujiji
Kigoma Ujiji

Mahali pa Kigoma katika Tanzania

Majiranukta: 4°52′48″S 29°36′36″E / 4.88000°S 29.61000°E / -4.88000; 29.61000
Nchi Tanzania
Mkoa Kigoma
Wilaya Manisipaa ya Kigoma Ujiji
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 232,388
Barabara Kuu ya Kigoma
Kigoma mjini (pamoja na Ziwa Tanganyika na kituo cha reli) (picha ya Tamino Boehm)
Kaiser House

Kigoma Ujiji ni manispaa katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania na makao makuu ya mkoa huo yenye msimbo wa posta 47100. Inaunganisha miji ya kihistoria ya Ujiji na Kigoma. Manispaa hii ilikuwa na wakazi wapatao 215,458 wakati wa sensa ya mwaka 2012.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 wazazi walihesabiwa 232,388 [2].

Kigoma na Ujiji iko kando ya Ziwa Tanganyika, magharibi mwa Tanzania.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ujiji ni kati ya miji ya kale zaidi katika Tanzania bara. Ilikuwa kituo kikuu cha njia ya misafara iliyofika hapa kutoka miji ya pwani kama vile Bagamoyo, Saadani au Pangani. Kutoka hapa bidhaa kama pembe za ndovu na watumwa kutoka Kongo na Tanzania bara zilipelekwa tena pwani.

Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kijerumani Ujiji ilikuwa pia mahali pa makampuni ya Kizungu na makao makuu ya Mkoa wa Ujiji katika utawala wa koloni[3].

Tangu kufikia kwa meli za kisasa ikaonekana ya kwamba mwambao wa Ujiji haukufaa sana kwa meli na hivyo mji mpya ulianzishwa kwenye hori la Kigoma karibu na Ujiji. Mji mpya ya Kigoma ukakua haraka ukawa pia kituo kikuu cha Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam iliyokamilishwa mwaka 1914 miezi michache kabla ya

Mji ulianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kwenye rasi ndogo inayoingia katika maji ya Ziwa Tanganyika na kuwa na nafasi ya bandari kwa meli za ziwani. Hapa ilikuwa pia mwisho wa Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam.

Baada ya kukamilishwa kwa njia ya reli katia Februari 1914 vipande vya meli mpya Goetzen vilifika Kigoma kutoka Ujerumani vikaunganishwa hapa. Meli hii ilizamishwa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, ikafufushwa tena na inahudumia bandari za Ziwa Tanganyika hadi leo kwa jina la "Liemba".

Masimulizi juu ya Kigoma Ujiji

[hariri | hariri chanzo]

Wakati miji kadhaa ya Afrika ikipata majina kutokana na ujio wa wageni, kuna baadhi ya miji ilipata majina yake kutokana na Waafrika wenyewe. Kutaja majina kutokana na wenyeji kulitegemea sana watu, hasa wale waliokuwa maarufu kwenye jamii. Kumbe ile miji iliyopata majina kutokana na wageni, sababu ilikuwa ni kujiwekea sifa kwa mataifa hayo na wakati mwingine mitazamo tu ya wageni hao ilisababisha mji fulani kupata jina.

Kwa upande wa miji kama Ujiji na Kigoma, watu huamini kuwa miji hiyo ilikuwa kipindi cha ukoloni. Ukweli ni kwamba Ujiji na Kigoma ilipata kukua kwa muda mrefu sana hata kabla ya ujio wa wageni kwenye maeneo hayo.

Kihistoria miji hiyo ilipata majina kutokana na watu maarufu waliopata kuishi na kujiwekea historia katika miji hiyo.

Watu wengi hudhani kuwa mji wa Kigoma na Ujiji ilianzishwa na ndugu wawili waliofahamika kwa majina ya Kajiji na Kagoma (Bugoye).

Ifahamike tu kwamba kabla ya mji wa Kigoma kuitwa Kigoma palikuwa panaitwa Lusambo_Gwa_Nyange na Ujiji palikuwa panaitwa Ubujiji.

Inaelezwa kuwa Kajiji alikuwa mkarimu, mpole na mwenye upendo kwa watu wote, na Kagoma alionekana kuwa tofauti kwa jamii. Kutokana na tabia hizo za ndugu hao wawili, wengi walimpenda sana Kajiji na kufanya maeneo aliyokuwa akiishi kupendwa na watu wengi. Kwa kuwa idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka, basi walipokuwa wakienda kwa Kajiji wakasema tunaenda Ubujiji kulingana na lugha ya kikabila.

Wengi walikuwa wanapenda kwenda Ubujiji na kujikuta wakijazana kwenye mji huo. Hata wageni walipoingia kwenye karne ya 19, walikuta mji huo una idadi kubwa sana ya watu. Kwa kuwa wakati huo Waarabu hawakuwa na nguvu sana hawakutaka kubadilisha jina hilo na badala yake waliamua kuendeleza mji huo na jina hilo.

Mpaka ukoloni ukianzishwa bado eneo hilo lilikuwa na jina hilo, isipokuwa kukawa na mabadiliko katika orthografia na matamshi ya neno Ubujiji, ndipo tukapata jina Ujiji na hata kwenye maandiko ya wakati huo mji huo ulitambulishwa kama Ujiji.

Kwa upande wa Kagoma au Bugoye pia mambo yalikuwa hivyo, sema kwa upande wa Kagoma, mji ulipata kukua kutokana na ujio wa Wagoma katika mji wa Kagoma.

Ikumbukwe kuwa Wagoma ni moja ya makabila ya Kimanyema waliokuja Tanganyika kipindi cha ukoloni karne ya 18. Sultani wa Wagoma alikuwa akiitwa Sultani Simba.

Mara baada ya Wagoma hao kusikia mji huo unaitwa Kigoma, walijisikia raha sana kwani mji ulikuwa unafanana na jina la kabila lao, hivyo kujikuta wakiupenda na kuanza kuujenga. Ile sehemu aliyokuwa akikaa Kagoma au Bugoye palifahamika kwa jina la Ibugoye ambapo kwa sasa ndio pale Mwanga. Lakini kiuhalisia Wagoma walifikia maeneo ya Bangwe.

Kwa kuwa ardhi ya Ujiji ilikuwa yenye rutuba, Wagoma walipenda kulima maeneo ya Ujiji. Kwa hiyo mji wa Kigoma na Ujiji ni miji ambayo ilijipatia historia ya pekee barani Afrika, kwani miji hiyo imepata majina yenye asili yake hapahapa.

Ikumbukwe kwamba Wagoma ni kabila la Wamanyema, kwa sababu Wamanyema ni mkusanyiko wa makabila zaidi ya 18 yaliyoungana na kuwa kitu kimoja.

Pia Wamanyema walipofika Kigoma kuna ambao walipata majina katika miji kama Katonga, Kabwe, Mkabogo au Kabogo: hao wote walikuwa Wamanyema wenye asili ya Kongo.

Pia Waha waliokuwa Kigoma na Ujiji waliwapokea watani wao Wamanyema na kuanza kuishi pamoja mpaka sasa.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-05. Iliwekwa mnamo 2014-01-13.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. Mwaka 1913 Ujiji ilikuwa na wakazi 25,000 na wengi wao wali kuwa Wamanyema. Mji ulikuwa na makampuni 9 za Waarabu, 7 za Wahindi na 2 za Wazungu. Kulikuwa pia na kituo cha kikosi cha 6 cha jeshi la Schutztruppe. (ling. Kamusi ya Koloni za Kijerumani, "Udjidji")
Kata za Wilaya ya Kigoma Mjini - Mkoa wa Kigoma - Tanzania

Bangwe | Buhanda | Businde | Buzebazeba | Gungu | Kagera | Kasimbu | Kasingirima | Katubuka | Kibirizi | Kigoma | Kipampa | Kitongoni | Machinjioni | Majengo | Mwanga Kaskazini | Mwanga Kusini | Rubuga | Rusimbi

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kigoma-Ujiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.