Musoma (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Musoma

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Tanzania" does not exist.Mahali pa mji wa Musoma katika Tanzania

Majiranukta: 1°29′24″S 33°48′0″E / 1.49°S 33.8°E / -1.49; 33.8
Nchi Tanzania
Mkoa Mara
Wilaya Musoma Mjini
Idadi ya wakazi
 - 108 242
Msimbo wa posta 31101 - 31113  

Musoma ni mji wa Tanzania uliopo kwenye mwambao wa mashariki wa Ziwa Viktoria. Musoma imepata halmashauri na hadhi ya manisipaa. Manispaa hiyo inapakana na Wilaya ya Musoma Vijijini.

Ni makao makuu ya Mkoa wa Mara.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa mji huo ilihesabiwa kuwa 108,242 [1].

Tembo beach.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ukoloni eneo la Musoma lilikuwa nchi ya Wakabwa, kundi la Wajaluo waliowahi kuhamia hapa.[2]

Wajerumani wa kwanza walifika mnamo mwaka 1910: walikuwa wamisionari, kwa majina Dominik na Paulo, waliojenga makazi na shule karibu na makao ya Mtemi Nyabange[3].

Wakafuatwa na afisa wa kwanza Mjerumani aliyeitwa na wenyeji "Bwana Sirusi" mwenye kazi ya afisa forodha. Huyu Sirusi alihamia mahali pa Musoma ya leo kwa sababu huko kina cha maji ufukoni kilifaa zaidi kwa meli kufika[4]. Hivyo Musoma ilianzishwa kama bandari na baadaye makao ya ofisa mdogo wa Mkoa wa kikoloni wa Mwanza.

Baada ya kuondolewa kwa Wajerumani, Waingereza waliingia. Katika eneo la kudhaminiwa la Tanganyika Musoma ilikuwa makao makuu ya wilaya (district) ikaingia vile katika Tanzania huru.

Mwalimu Julius Nyerere alisoma shule hapa Musoma kuanzia mwaka 1934 na tarehe 21 Januari 1953 alirudi hapa kufunga ndoa na Maria Waningu Gabriel Magige katika Kanisa Katoliki la Musoma Mwisenge [5].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Matokeo ya sensa ya 2002 kwa mkoa wa Mara. Jalada kutoka ya awali juu ya 2003-12-18. Iliwekwa mnamo 2003-12-18.
 • Siso - Shetler, uk. 75
 • Kutokana na maelezo katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani Nyabange iliyoitwa "Njawangi" (jer. "j"=y) ilikuwapo takriban kilomita 10 upande wa mashariki wa Musoma kwenye mwambao wa hori ya ziwa, angalia makala "Muansa" na "Njawangi" katika kamusi hii
 • Siso - Shetler, uk. 79
 • Thomas Molony, Nyerere: The Early Years , Boydell & Brewer Ltd, 2014 , uk. 189
 • Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  Flag of Tanzania.svg Kata za Manisipaa ya Musoma - Mkoa wa Mara - Tanzania Flag of Tanzania.svg

  Buhare | Bweri | Iringo | Kamunyonge | Kigera | Kitaji | Makoko | Mukendo | Mwigobero | Mwisenge | Nyakato | Nyamatare | Nyasho


  Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
  Je unajua kitu kuhusu Musoma (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
  Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
  Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

  Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.