Wikipedia:Mwongozo (Anzisha makala)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Kama makala fulani haiko bado unweza kuianzisha.

Maswali kabla ya kuanzisha

Kabla ya kuianzisha ujiulize maswali yafuatayo:

 1. Je ni afadhali kuanzisha makala mpya badala ya kuongeza makala iliyopo tayari?
 2. Je una uhakika ya kwamba makala hii haiko bado? Labda kwa jina tofauti kidogo ? (Mfano: Westlands haiko, lakini kuna Westlands (Nairobi)). Lazima uchungulia kwa kutafuta jina kwa njia ya dirisha la kutafuta sehemu ya pili (ukitaipu "A" utaona kwanza orodha ya makala yanaoanza kwa "A" kama Afrika, Afrika Kusini, Asia - na chini yake "ya maneno...". Hapo chini unapata makala yote yenye neno unalotumia.
 3. Je ni kweli makala inayofaa kwa wikipedia? Angalia Wikipedia:Umaarufu. (Mifano: makala juu ya shangazi yako haina mahali hapa kama shangazi huyu hajulikani nje ya ukoo na kijiji chake; makala inayoeleza neno fulani si kazi ya wikipedi lakini wikikamusi...)

Kuandaa makala

Unatakiwa kuandaa makala yako ili kuwa na habari za maana na viungo vya lazima.

 • Panga maandishi yako. Utangulizi inayojumisha habari za kimsingi katika sentensi 1-3, baadaye habari za undani zaidi.
 • Tafuta kurasa za marejeo katika intaneti (=kurasa zenye habari za maana zitakazotajwa chini ya makala)
 • Kumbuka pia makala yanayoweza kuhusiana na makala yako; uliweza kuziona (kama zipo) kwa kutumia dirisha la kutafuta jinsi ilivyoelezwa hapo juu na. 2. Ni vema kuweka viungo kadhaa kwa makala za maana. Mfano: Unaandika juu ya mtaa wa Daressalaam. Hapa ni lazima kuwega viungo kwa jina la mji, labda mitaa mingine muhimu iliyotajwa tayari, jina la wilaya yake, labda majengo au taasisi muhimu zilizopo hapa. Haitoshi kutaja majina haya, lazima kuweka viungo kwa umbo sahihi.
 • Tafuta pia kama makala ya Kiingereza iko juu ya kichwa chako. Mara nyingi iko, na hapo utaifungua na kukopi orodha ya interwiki na kuibandika chini ya makala mpya.
 • Soma orodha ya makosa ya kawaida na uepukane nayo.


Kuanzisha makala


 1. Kwanza kabisa ujiandikishe yaani uhakikishe ya kwamba una akaunti ya jina lako na umeingia kwa jina lako - si lazima lakina tunakushauri ufanya hivyo!
 2. Andika jina la makala katika uwazi upande wa kulia. Thebitisha kwa kubofya "Anzisha makala yenye jina hili".
 3. Sasa andika sentensi ya kwanza kwa namna ya kamusi: jina la makala kwa kawaida liwe neno la kwanza / maneno ya kwanza na kuonekana kwa herufi koza.
 4. Mlango unaofuata katika mwongozo huu unakuelezea namna gani kupanga umbo la makala.
 5. Chini ya makala weka sehemu ya "Vyanzo" au "Marejeo" na chini yake orodha ya interwiki uliyokopi kutoka wikipedia ya lugha nyingine.
 6. Usisahau kupanga makala yako katika jamii inayofaa (yaani kundi la makala zinazojumuiwa na kichwa).
 7. Bofya "Onyesha hakikisho la mabadiliko" na sasa unaona umbo la makala jinsi itakavyoonekana.
 8. Fanya masahihisho ya lazima halafu bofya "Hifadhi ukurasa".
 9. Sasa fungua tena dirisha la hariri na kuingiza viungo kwa makala zilizopo tayari zinazohusiana na makala mpya (taz. juu).
 10. Anzisha kila mstari mpya kwenye nafasi ya kwanza. Usiache nafasi tupu mwanzoni mwa mstari mpya. Hii italetata matatizo itaonekana hivyo itasomeka vibaya:
    Anzisha kila mstari mpya kwenye nafasi ya kwanza. Usiache nafasi tupu mwanzoni mwa mstari mpya. Hii italetata matatizo itaonekana hivyo itasomeka vibaya. Hatuitaki hapa.

Baada ya kuandika

Makala ilyioanzishwa nawe iko katika orodha ya "Maangalizi yangu" (unaona kiungo chake juu ya kila dirisha la wikipedia kama umeingia; kama huioni hujaingia bado!). Uiangalie wakati mwingine na tazama kama wasomaji wengine waliandika maoni au ushauri kwenye ukurasa wa majadiliano. Hapa utaona pia kama kuna mtumaji amepinga maandisho yake, labda baada ya kuona kasoro nzito. Usisite kuwasiliana juu ya maoni haya.


Jaribu kuhariri katika sanduku la mchanga
Endelea mwongozo na Muundo