Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Mwongozo (Kumbuka)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Taratibu na kawaida kwenye wikipedia

Kuna machache ambayo unatakiwa kukumbuka ukichangia na kuhariri kwenye wikipedia.

Umuhimu: Kuandika juu ya nini?

Wikipedia ni kamusi elezo. Kwa hiyo tunalenga kukusanya habari zinazofaa kwa kamusi elezo. Maana yake makala yanatakiwa kuhusiana na mada yenye umuhimu fulani.

Wanawikipedia wanaendelea kujadiliana umuhimu ni nini. Kwa jumla tuko pamoja ya kwamba haifai kuwa na makala juu ya mtu yeyote anayeishi au aliyeishi duniani, au kuhusu kila barabara za miji yote au kuhusu kila kampuni inayouza kitu kwenye sayari hii. Kwa hiyo tutaendelea kujadiliana "umuhimu" ni nini ila tu ujiandae kutetea chaguo lako na usikate tamaa kama makala juu ya shangazi yako inafutwa na wengine !

Kamusi elezo si sawa na kamusi ya lugha. Kwa hiyo makala zinazoeleza maana ya neno tu si shabaha yetu. Kuna mradi ndugu wa Wikamusi kwa kamusi ya lugha ingawa ni changa bado.

Pia maandishi marefu kutoka kitabu -ama kitabu chako mwenyewe au kitabu kinachopatikana kama maandiko huria kwenye intaneti hayafai kuingizwa vile hapa wikipedia. Kuna mradi mwingine kwa maandishi ya aina hii ambao unaitwa Wikisource. Lakini nukuu fupi inakubalika.

Miradi ndugu ya wikipedia

Kuna miradi mingine iliyoanzishwa pamoja na wikipedia ingawa sehemu kubwa bado haiko kwa Kiswahili:

Commons
Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
Meta-Wiki
Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
Wikamusi
Kamusi na Tesauri
Wikitabu
Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
Wikidondoo
Mkusanyiko wa Nukuu Huria
Wikisource
Nyaraka Huru na za Bure
Wikispishi
Kamusi ya Spishi
Wikichuo
Jumuia ya elimu
Wikihabari
Habari Huru na Bure

Kwa orodha ya miradi yote tazama Complete list of Wikimedia projects kwa Meta.

Yasiyofaa

Wikipedia si mahali pa:

  • kuonyesha matokeo ya utafiti asilia yaani habari ambazo wewe kama mwandishi umebuni mara ya kwanza au nadharia mpya zisizoangaliwa bado na wataalamu wengine. Maana yake kama wewe umegundua ukweli fulani wikipedia si mahali pa kuitangaza mbele ya dunia. Tunapendelea kusubiri hadi wataalamu wengine wameiangalia na kuchangia mawazo yao.
  • kujitangaza. Kama wewe ni mwandishi, mwimbaji au msanii bora haifai ukieleza ubora wako mwenyewe. Subiri tu kidogo hadi wengine wanakujua na kuimba sifa zako!
    • Usianzishe makala juu yako mwenyewe katika sehemu ya kamusi! Unaweza kutumia nafasi ya ukurasa wako wa mtumiaji. Hapa uko huru kuleta habari juu yako. Nje ya hapo ni marufuku! (soma zaidi hapo: Wikipedia:Ukurasa wangu na kurasa za kamusi)
    • Usitaje jina lako katika makala kama mwandishi.
  • kutangaza biashara, kuhubiri juu ya dini au siasa
  • kutukana wengine.

Msimamo wa kutopendelea upande

Sheria muhimu katika wikipedia "Msimamo wa kutopendelea upande. Sheria hii inasema ya kwamba tunakubali kutaja maoni mbalimbali yenye maana juu ya mada fulani.

  1. Si mahali pa kumsifu au kumpinga mtu au kitu chochote. Si mahala pa kusambaza maoni kama ukweli.
  2. Ni sawa kutaja maoni lakini sharti maoni yaonekana vile tusiyaonyeshe kama ukweli halisi.
  3. Tusiandike: "Bwana fulani ni mwanamichezo bora wa Afrika". Hii ni hoja, si bayana ya hakika. Kama ni kweli na muhimu, andika ya kwamba "Kuna watu wanaomwona kama mwanamichezo bora wa Afrika". Lakini kama huwezi kutaja ushuhuda au vyanzo (taarifa ya gazeti inayopatikana katika intaneti au kitabu) kuwa amesifiwa hivyo uwezekano ni mkubwa ya kwamba sentensi kama hii itafutwa.
  4. Tujaribu kuchukua msimamo wa kati yaani tueleze mitazamo na maoni mbalimbali yaliyopo kama ni muhimu.

Msimamo huu ni muhimu hasa kwenye mada kama dini au siasa ambako maoni hutofautiana mara nyingi.

Kwa ushauri zaidi unaeza kuangalia majadilianoi kwenye wikipedia ya Kiingereza kama vile: Staying cool when the editing gets hot na pia Wikipedia:NPOV_tutorial.

Kutaja vyanzo

Kumbuka ukurasa wa Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo)!

Haki za hatimiliki

  • Usiingize picha au maandishi ambako mtu fulani ana hakimiliki bila kibali chake!
  • Usinakili na kumwaga maandishi kutoka tovuti nyingine katika makala! Tumia maneno yako mwenyewe. Hata maandishi ya intaneti huwa na haki za hatimiliki.
  • ukitafsiri makala ya wikipedia ya lugha nyingine au kuchukua picha kutoka huko ni halali.

Uungwana wa wikipedia

Wikipedia inaomba wachangiaji wote watendeane an kujadiliana kwa heshima. Hata kama mawazo yanatofautiana kumbuka hii!.

Wote hapa wanajitolea bila malipo. Ukimwona mtu akifanya jambo la ajabu au kosa umwandikie kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala na kwenye ukurasa wa majadiliano wa mtumiaji.

Linganisha Wikipedia:Etiquette.

Kubadilisha jina la makala ?

Wakati mwingine utakuta makala unapofikiri ya kwamba jina lake si sahihi. Ama mwandishi alikosa tahajia au jina lenyewe au kwako mada hii inajulikana zaidi kwa jina tofauti.

  1. Usinakili yaliyomo ya makala na kuiweka kwa makala mpya yenye jina nyingine!! Hii ni kosa kubwa. Hasa kwa sababu inafuta historia ya makala na viungo vilivyopo tayari.
  2. Unaweza kuhamisha makala kwenda jina jipya baada ya kutafuta majadiliano na wengine. Jaribu kupatana na wahariri wengine kwanza. Kwa hiyo unaandika hoja lako kwenye ukurasa wa majadiliano. Usisahau kutaja kifupi pendekezo lako kwenye mstari wa "muhtasari" (chini ya dirisha la kuhariri). Na angalia kwenye historia ya makala ni nani mhariri aliyetunga makala, unaweza kuchungulia kama yuko bado na kumwomba asome pendekezo lako.

Baadaye unaweza kuhamisha makala kwenda jina jipya kama umejiandikisha sawasawa. Heri usihamishe kurasa za "maana". (Linganisha en: How to rename (move) a page.

  1. Wakati mwingine njia inayofaa ni kuanzisha ukurasa wa kuelekeza. Hapa unafungua ukurasa mpya kwa jina unalofikiri ni sawa au afadhali ndani yake unaweka tu kielekezo. Mfano: Unakuta ukurasa wa nchi "Cote d'Ivoire"; unafikiri afadhali iwe "Aivori Kost" maana umeona umbo hili la jina. Basi unanzisha makala ya "Aivori Kost", na ndani yake unaandika tu
#REDIRECT [[Cote d'Ivoire]]
(unaweza pia kubofya alama ya na kuingiza jina la ukurasa husika uliopo tayari , katika mfano "Cote d'Ivoire". Kila anayetafuta "Aivori Kost" atafika "Cote d'Ivoire")

Kuonya na kubana

Kwa bahati mbaya tunakuta mara kwa mara wachangiaji wasiofuata ushauri na kuleta makala zisizolingana na kanuni zetu. Wakabidhi wa wikipedia hii wanajaribu kuwashauri, kama lazima pia kuwaonya. Wasipofuata maonyo, wanaweza kubanwa kwa muda fulani au milele. Wako pia watumiaji wanaoleta uharabu kwa kufuta maudhui au kuigiza upuuzi; wakionekana wamefanya haya kwa makusudi wanabanwa. Kila mwanawikipedia ana haki ya kupinga kama amebanwa. Kimsingi wakabidhi wanajaribu kufuata kanuni zinazoelezwa kwa Kiingereza hapa simple:Wikipedia:Blocks_and_bans (kwa kifupi katika simple.wikipedia) au hapa en:Wikipedia:Blocking_policy (kwa kirefu, enwiki). Orodha ya waliobanwa inaonekana hapa Maalum:Kumbukumbu/block.