Wikipedia:Mwongozo (Kujisajili)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    
Bofya hapa - kona ya juu upande wa kulia
Dirisha unaloona ukibofya "Create account / Kujisajili"

Kujisajili kama mtumiaji

Kila mtu anaweza kuchangia kwenye Wikipedia hata bila kujiandikisha.

1. Faida za kujisajili

Kujisajili kunaleta nafasi za nyongeza na faida hasa ukichangia mara kwa mara. Hasa:

  • unapata nafasi zaidi za kuhariri, kwa mfano kama ukurasa umehifadhiwa
  • unapata ukurasa wa "Maangalizi yangu" unaosaidia kutazama makala unazopenda kufuatilia.
  • unaweza kuhamisha kurasa (lakini kumbuka sheria zake)
  • ni rahisi kutambuliwa na kuheshimiwa na wengine kwa sababu wanakujua kutokana na michango yako
  • wengine wanaweza kuwasiliana nawe kwenye ukurasa wako wa majaidiliano

2. Kufungua akaunti

  • Hatua ya kwanza ni kubofya kwenye kona ya juu na baadaye tena kwa "kujisajili".
  • Kwa usalama wa Wikipedia ni lazima kutaipu herufi zinazoonyeshwa katika dirisha dogo chini yake.
  • Sasa unaingiza jina ulivyojichagulia na nywila (neno lako la siri) mara mbili.
  • anwani ya baruapepe si lazima; lakini unashauriwa kuiandikisha! Inasaidia kama unapenda kuwasiliana na watumiaji wengine kwa njia hiyo. Unaweza pia kuiacha kwanza na kuiongeza baadaye.
  • Mwishoni unabofya chini "sajili akaunti"
  • Kama jina ulilochagua limeshachukuliwa na mwingine au kama umekosea kutaipu neno la siri mara mbili unaona dirisha unapaswa kuanza upya.

3. Kuingia

  • Ukiwa mwenye akaunti na jina la Wikipedia unaweza kuingia kila safari unapofungua Wikipedia.
  • Unabofya tena kwenye kona ya juu utapata dirisha la "Ingia".
  • Sasa unaona viungo vipya kwenye mstari wa juu kabisa kama vile
    • Jina lako - inafungua ukurasa wako binafsi
    • Majadiliano yangu - inafungua majadiliano kwenye ukurasa wako
    • Mapendekezo yangu - hapa unaweza kubadilisha kuonekana kwa kurasa zako
    • Maangalizi yangu - inaonyesha orodha ya makala uliyochagua kufuatilia mabadiliko yao
    • Michango yangu - inakupa orodha ya michango yote uliyofanya kwenye Wikipedia
    • Toka - ukipenda kutoka kwa safari hii - baada ya kubofya hutakuwepo tena kwa jina hadi kuingia tena
  • Kama mwandishi aliyejiandikisha utaonekana kwa watumiaji wote wengine - kwa mfano hivyo: Bofya hapa na andika jina la mtumiaji

4. Kuwezesha baruapepe

  • Hakikisha kwamba umeingiza anwani yako ya baruapepe
  • Bofya menyu "Mapendekezo" ("preferences")
  • Tafuta chini "Hitiari za barua pepe"
  • Bofya "Yakinisha anwani yako ya barua pepe"
  • Sasa fungua baruapepe zako, utaona ujumbe kutoka Wikipedia / Wikimedia.org
  • Thibitisha kwa kubofya "Confirm email address"
  • Sasa kila mtumiaji aliyejiandikisha ataona menyu "Email this user" kwenye ukurasa wako. Anaweza kukuandikia lakini haoni anwani yako.