Wanawake Watetezi Wa Haki za Binadamu
Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu (kwa Kiingereza: Women Human right defenders) ni wanawake wanaotetea haki za binadamu hususani haki zote za wanawake zinazohusiana na jinsia na jinsi[1][2][3] ingawa si zote zinakubalika kimataifa, kwa mfano utoaji mimba unatazamwa na nchi mbalimbali kuwa hauwezi kuwa haki ya yeyote kwa sababu unapingana na haki ya kuishi aliyo nayo mtoto.
Licha ya kukumbana na changamoto nyingi katika kazi zao zinatambulika na maazimio ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2013, ambayo yanahitaji uwepo wa ulinzi mahususi kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu.[4]
Mwanamke mtetezi wa Haki za binadamu anaweza kuwa ni mzawa anayepigania haki kwa ajili ya jamii yake, mwanamke anyepambana na vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali.
Kama ilivyo kwa watetezi wengine wa haki za binadamu, wanawake watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuwa walengwa wa mashambulizi kutokana na jitihada zao za kudai haki itendeke. Huweza kukutana na matatizo ya kutengwa, kutukanwa, kutishiwa na ukatili wa aina mbalimbali kutoka kwenye jamii zao. Wanaweza kukutana na vikwazo fulani kutegemea na nafasi yao na wanachotetea.
Siku ya Wanawake watetezi wa haki za binadamu imekuwa ikiazimishwa kila mwaka tarehe 29 Novemba tangu mwaka 2006.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "About WHRDIC |". www.defendingwomen-defendingrights.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-14. Iliwekwa mnamo 2018-05-13.
- ↑ "Women Human Rights Defenders", AWID, 2014-12-17. Retrieved on 2023-01-18. (en) Archived from the original on 2018-05-14.
- ↑ "Report of the Special Rapporteur on the situation of human rights defenders, Margaret Sekaggya (2010)". www.un.org. Iliwekwa mnamo 2018-05-13.
- ↑ "UN adopts landmark resolution on Protecting Women Human Rights Defenders", ISHR. (en)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |