Nenda kwa yaliyomo

Patrick Mfugale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Patrick Aron Lipilima Mfugale (Ifunda, mkoa wa Iringa [1], 1950 - 29 Juni 2021) alikuwa mhandisi maarufu nchini Tanzania, mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Barabara nchini Tanzania TANROADS.[2]

Mfugale alimaliza elimu ya upili katika shule ya Moshi mwaka 1975. Alipata shahada ya kwanza ya uhandisi mwaka 1983 kutoka Chuo Kikuu cha Rokii (Uhindi) iliyofuatwa na shahada ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Loughborough (Uingereza) mwaka 1995.

Mwaka 2003 alipokea tuzo ya Bodi ya Wahandisi wa Tanzania na mwaka 2018 alipokea tuzo nyingine iitwayo "Engineering Execellency". Patrick Mfugale alitengeneza mfumo wa usimamizi madaraja uitwao "Bridge Management System".

Katika mradi wa barabara za juu nchini Tanzania, serikali iliamua kulipa daraja moja jina Daraja la Mfugale.

Mfugale amefariki dunia mwezi Julai 2021

Madaraja aliyojenga

[hariri | hariri chanzo]

Mfugale amefanikiwa kusimamia ujenzi jumla ya madaraja elfu moja na mia nne[3], yafuatayo ni madaraja machache aliyosimamia:

  1. "Je Patrick Mfugale ni nani?", BBC News Swahili, 2018-09-27, iliwekwa mnamo 2020-02-09
  2. "TANROADS Official Website :: Chief Executive Message". www.tanroads.go.tz. Iliwekwa mnamo 2020-02-09.
  3. Mfahamu mhandisi Patrick Mfugale 'kichwa' nyuma ya flyover ya Tazara, tovuti ya nukta.co.tz ya tar. Septemba 27, 2018
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Patrick Mfugale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.