Daraja la Julius Nyerere
Mandhari
Daraja la Kigamboni English: Kigamboni Bridge | |
---|---|
Mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek) | |
Yabeba | Leni 6 |
Yavuka | Mkondo wa Kurasini |
Mahali | Dar es Salaam, Tanzania |
Mmiliki | NSSF (60%) Serikali ya Tanzania (40%) |
Mbunifu wa mradi | Arab Consulting Engineers |
Aina ya daraja | Daraja la kuning'inia (Cable-stayed bridge) |
Urefu | mita 680 |
Upana | mita 27.5 |
Mjenzi | China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company |
Ujenzi ulianza | Februari 2012 |
Gharama za ujenzi | US$ 136 milioni |
Badala ya | Kivuko cha MV Magogoni |
Anwani ya kijiografia | 6°51′36.25″S 39°17′56.31″E / 6.8600694°S 39.2989750°E |
Daraja la Kigamboni ni daraja ambalo linavuka mkondo wa Kurasini jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Daraja hilo lina urefu wa mita 680, upana wa mita 32 na njia sita za kupitisha magari. Ndilo daraja kubwa katika Afrika ya Mashariki. Lilizinduliwa rasmi tarehe 19 Aprili 2016 na rais John Magufuli na kupewa jina "Daraja la Julius Nyerere" kwa heshima ya rais wa kwanza wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere.
Daraja hili limechukua nafasi ya feri iliyosafirisha watu na magari kati ya kata za Kigamboni na Kurasini upande wa jiji. Njia nyingine ya kuvuka bado ni feri kati ya Kigamboni na Kivukoni.
Makala hii kuhusu daraja barani Afrika bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |