Daraja la Selander
Jump to navigation
Jump to search
Daraja la Selander Kiingereza: Selander Bridge | |
---|---|
Yabeba | Barabara ya Ali Hassan Mwinyi (leni 4) |
Yavuka | Mkondo wa Msimbazi (Msimbazi Creek) |
Mahali | Oyster Bay, Dar es Salaam |
Mmiliki | Serikali ya Tanzania |
Urefu | mita 85 |
Kilifunguliwa | 1929 |
Anwani ya kijiografia | 6°47′46.69″S 39°16′52.81″E / 6.7963028°S 39.2813361°E |
Daraja la Selander ni daraja kwenye Barabara ya Ali Hassan Mwinyi (Bagamoyo Road) ambalo linavuka mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Daraja hili lilitengenezwa mwaka 1929 likapewa jina kwa kumbukumbu ya John Einar Selander aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa ujenzi katika eneo la Tanganyika chini ya utawala wa Waingereza.[1]
Daraja hili lilipanuliwa na Japan International Cooperation Agency mnamo 1980[2] kuwa na njia 4 za magari.
Tangu mwaka 2019 daraja la pili limeanza kujengwa takriban mita 300 kando yake upande wa Oyster Bay.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ (2007) Dar es Salaam: Histories from an Emerging African Metropolis. Page 104, Mkuki na Nyota. Retrieved on 7 March 2013.
- ↑ 30 Years Of JICA Tanzania Office (1980-2010) (PDF). Page 6, Japan International Cooperation Agency (2010). Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 7 March 2013.
|
![]() |
Makala hii kuhusu daraja barani Afrika bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |