Daraja la Julius Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Daraja la Kigamboni)
Daraja la Kigamboni
English: Kigamboni Bridge
Mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek)
YabebaLeni 6
YavukaMkondo wa Kurasini
MahaliDar es Salaam, Tanzania
MmilikiNSSF (60%)
Serikali ya Tanzania (40%)
Mbunifu wa mradiArab Consulting Engineers
Aina ya darajaDaraja la kuning'inia
(Cable-stayed bridge)
Urefumita 680
Upanamita 27.5
MjenziChina Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company
Ujenzi ulianzaFebruari 2012
Gharama za ujenziUS$ 136 milioni
Badala yaKivuko cha MV Magogoni
Anwani ya kijiografia6°51′36.25″S 39°17′56.31″E / 6.8600694°S 39.2989750°E / -6.8600694; 39.2989750
Daraja la Julius Nyerere is located in Tanzania
Daraja la Julius Nyerere
Mahali ya daraja nchini Tanzania

Daraja la Kigamboni ni daraja ambalo linavuka mkondo wa Kurasini jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Daraja hilo lina urefu wa mita 680, upana wa mita 32 na njia sita za kupitisha magari. Ndilo daraja kubwa katika Afrika ya Mashariki. Lilizinduliwa rasmi tarehe 19 Aprili 2016 na rais John Magufuli na kupewa jina "Daraja la Julius Nyerere" kwa heshima ya rais wa kwanza wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere.

Daraja hili limechukua nafasi ya feri iliyosafirisha watu na magari kati ya kata za Kigamboni na Kurasini upande wa jiji. Njia nyingine ya kuvuka bado ni feri kati ya Kigamboni na Kivukoni.

Nyerere Bridge huko Kigamboni, Dar es Salaam, ni daraja pekee la Afrika Mashariki lisilo na nguzo majini.