Nenda kwa yaliyomo

Ifunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ifunda ni kata ya Wilaya ya Iringa katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51212.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 18,420 na idadi hii inazidi kuongezeka kutokana na ujenzi wa miundombinu na shughuli mpya za kiuchumi, vikiwemo viwanda hali kadhalika ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Iringa[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,199 waishio humo.[2]

Ifunda ni sehemu muhimu katika maendeleo ya elimu katika mkoa na taifa kiujumla; hii ikichagizwa na uwepo wa taasisi za kielimu kama:

  • 1. shule ya sekondari ya ufundi Ifunda
  • 2. shule ya sekondari ya wasichana Ifunda (zamani Ifunda Teachers College)
  • 3. shule ya sekondari Lyandembela
  • 4. chuo cha ufundi stadi Ifunda
  • 5. Ifunda Mission Vocational Training
  • 6. shule ya msingi Ifunda pamoja na shule nyingine za msingi zipatazo 12
Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ifunda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.