Asteroidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Asteoridi)
Rukia: urambazaji, tafuta
253 Mathilde ni asteroidi yenye vipimo vya 66×48×46 km
Ukanda wa asteroidi katika mfumo wa jua letu

Asteroidi (kutoka Kigiriki ἀστήρ aster = nyota na είδες -eides= ya kufanana) ni kiolwa cha angani kinachozunguka jua kama sayari. Ni ndogo kuliko sayari kibete lakini kubwa kushinda kimondo. Mara nyingi huitwa pia "planetoidi" kwa sababu tabia zao zinalingana katika mengi na sayari.

Katika mfumo wa jua letu kuna angalau asteroidi 338,000 zilizotambuliwa hadi leo na wanaastronomia. Nyingi zinazunguka katika ukanda wa asteroidi kati ya njia za Mirihi (Mars) na Mshtarii (Jupiter). Wataalamu hutofautiana kati yao kama hizi ni ama mabaki ya sayari iliyolipuka au vipande vya sayari ambayo haikukamilika bado.

Ukubwa wa asteroidi ni kati ya kipenyo cha kilomita 1,000 hadi sentimita kadhaa.

Tangu mwaka 2006 umoja wa kimataifa wa wanaastronomia umeamua kutofautisha kati ya asteroidi na sayari kibete. Sayari kibete ni gimba mango kubwa lenye masi ya kutosha kufikia umbo la tufe. Kutokana na mapatano haya violwa vilivyohesabiwa kama asteroidi kubwa kama Ceres siku hizi huitwa sayari kibete.

Majina ya asteroidi huwa na na namba mbele na jina linaloweza kupendekezwa na mfumbuzi wake. Asteroidi ya kwanza iliyogunduliwa ilikuwa 1 Ceres. Namba zinatolewa mfululizo na zinaonyesha nafasi yake katika historia ya ufumbuzi wa asteroidi. Leo hii takriban lakhi 2.5 zimepewa majina ya aina hii.

Hatari kutokana na asteroidi zinazokaribia dunia[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya dunia asterodi zimewahi kugonga dunia yetu mara kadhaa. Kama asteroidi inaelekea karibu na obiti ya dunia inaitwa kiolwa cha kukaribia dunia. Katika historia ya dunia migongano ilikuwa na athira kubwa na kusababisha mara kadhaa vifo vya spishi nyingi. Kutoweka kwa dinosauri inaaminiwa lilisababishwa na asteroidi kubwa iliyogonga uso wa dunia katika eneo la Yucatan huko Meksiko.

Katika miaka iliyopita taasisi za usafiri wa anga la nje kama NASA na ESA zimeanza utafiti wa undani kuhusu hatari hiyo na kupanga majaribio jinsi gani kulenga asteroidi mbali na dunia. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. How to stop an asteroid hitting earth, Guardian Tuesday 30 June 2015
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asteroidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.