Asha-Rose Mtengeti Migiro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asha-Rose Migiro
Migiro pamoja na Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon.

Asha-Rose Mtengeti Migiro (* 1956) aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Alipewa cheo hicho na Katibu Mkuu Ban Ki-moon tarehe 5 Januari 2007.[1]

Hadi kuteuliwa kwa cheo cha UM alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania tangu Januari 2006. Wajibu huo alipewa na rais Jakaya Kikwete aliyemteua kumfuata katika Wizara ya mambo ya nje iliyoshikwa awali na Kikwete mwenyewe.

Chini ya rais Benjamin Mkapa Migiro alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Alikuwa mbunge kwa njia ya kiti maalumu cha wanawake.

Kabla ya kujiunga na siasa alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alisoma Shahada ya Awali na Shahada ya uzamili hukohuko Dar es Salaam[onesha uthibitisho][2]

Mwaka 1992 akaongeza Shahada ya udaktari wa sheria kwenye Chuo kikuu cha Konstanz (Ujerumani). Akarudi Tanzania alipoanza kufundisha. Akawa mwanachama wa CCM.

Akiwa Mwislamu aliolewa na Cleophas Migiro; wana watoto wawili wa kike[onesha uthibitisho].[3]

Kwa sasa Asha Rose Migiro ameteuliwa kuwa waziri wa katiba na sheria wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Pia ni mke wa Ritchie Lunyonga[onesha uthibitisho].

Viungo vya Nje

Marejeo

  1. Asha-Rose Migiro | Tanzania Foreign Ministry Official List. www.tzembassy.go.tz. Iliwekwa mnamo 2020-08-21.
  2. University of Dar es Salaam-. www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2020-08-21.
  3. Jeff Msangi. DR.ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO. – Bongo Celebrity (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-02-25. Iliwekwa mnamo 2020-08-21.