Abu Dhabi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Abu Dhabi


Jiji la Abu Dhabi
Nchi Falme za Kiarabu
Jiji la Abu Dhabi kutoka angani (Machi 2003)

Abu Dhabi (kwa Kiarabu: أبو ظبي ʼAbū Ẓaby) ndio ufalme mkubwa zaidi katika Shirikisho la Falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni; pia ni jina la mji mkuu wa ufalme huu na wa shirikisho lote.

Mji umejengwa kwenye kisiwa karibu na mwambao.

Hadi 1970 ilikuwa mji mdogo wa nyumba za matofali ya matope. Tangu kupatikana kwa pesa ya mafuta mji ulikua kupita kiasi na nyumba zote ni mpya. Mwaka 2000 palikuwa na wakazi wapatao 1,000,000. Wakazi walio wengi sana (80%) si tena wazawa bali wageni, hasa kutoka Asia ya Kusini.

Maji matamu hutengenezwa kutokana na maji ya chumvi ya bahari.

Kuna mji wa pili katika ufalme: Al Ain yenye wakazi 348,000 (sensa ya mwaka 2003). Mji wa Ruwais ulianzishwa jangwani kabisa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Abu Dhabi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.