Nenda kwa yaliyomo

Najd

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Najd na mikoa yake katika Ufalme wa Saudia.

Najd, pia Nejd (kwa Kiarabu: نجد ), ni eneo kwenye kitovu cha Bara Arabu na pia katikati ya Ufalme wa Uarabuni wa Saudia.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Eneo hilo lina km² milioni 1.1. Limepakana upande wa magharibi na Hijaz, upande wa kaskazini na jangwa la Nefud, upande wa mashariki na Al-Hasaah, na upande wa kusini na jangwa la Rub al-Khali.

Tabianchi ni yabisi sana hivyo eneo lote ni jangwa. Watu huishi kwenye oasisi pekee. Kwa jumla kuna wakazi milioni 7 katika sehemu hizo, wengi wao katika jiji la Riyad ambalo ni mji mkuu wa Saudia. Miji mikubwa ni Riad (wakazi milioni 5,7), Buraidah (wakazi 500,000), Unaizah (takriban 140,000) na Ar Rass (takriban 120,000)[1].

Ugawaji wa kisiasa

[hariri | hariri chanzo]
Ramani Mkoa Kiarabu Mji mkuu Eneo
km²
Idadi ya watu
2004   1)
wiani majimbo
Ha'il حائل Ha'il 103,887 527,033 5.1 4
al-Qasim القصيم Buraida 58046 1016756 17.5 11
ar-Riyad الرياض Riad 404,240 5455363 13.5 20
1) Matokeo ya awali ya sensa ya 15. Septemba 2004
Falme za Najd na Hejaz jinsi zilivyokuwa kabla ya maungano wa Uarabuni wa Saudia.
Mitelemko ya Tuwaiq (karibu na Riyad).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Najd ilikuwa chanzo cha harakati ya Wahabiya tangu karne ya 18 walioshikamana na nasaba ya Saud[2].

Mwaka 1744 kiongozi wa kikabila Muhammad bin Saud aliungana na kiongozi wa kidini Muhammad ibn Abd al-Wahhab na umoja huo wa familia ya Saud na kundi la kidini la Wahabiya uliunda utawala wa kwanza wa Wasaudi juu ya Riad na sehemu za Najd.

Tangu 1818 Wasaudi walishindwa katika Najd na jeshi la Waturuki Waosmani; mwaka 1891 walipaswa kuondoka Najd na kukimbilia Kuwait.

Lakini mwaka 1902 Abdul Aziz Ibn Saud alifaulu kuvamia tena Riad na kuimarisha utawala wake huko. Wakati wa Vita Kuu ya kwanza hakushiriki katika vita ya Waarabu dhidi ya Waosmani, badala yake alishindana na makabila ya Najd ambayo hawakumtambua kama mkuu.

Mwaka 1921 aliweza kujitangaza kama Emir wa Najd. Hapo alivamia ufalme wa Hijaz akaushinda na mwaka 1926 Ibn Saud alijitangaza kuwa mfalme wa Hijaz. Mwaka uliofuata alianza kutumia cheo cha mfalme pia kwa Najd. Baada ya kutawala sehemu hizo mbili kwa namna ya pekee alitangaza maungano ya falme zote mbili kwenye mwaka 1932 akaanzisha Ufalme wa Uarabuni wa Saudia[3].

  1. جريدة الرياض – عين على القصيم Ilihifadhiwa 29 Julai 2013 kwenye Wayback Machine. (Tovuti ya alriyadh.com)
  2. History of Arabia, tovuti ya Encyclopedia Britannica
  3. The Saud Family and Wahhabi Islam, Helen Chapin Metz, ed. Saudi Arabia: A Country Study. Washington: GPO for the Library of Congress, 1992
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Najd kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.