Riyad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muonekano wa Mji wa Riyad

Riyad (Kar.: الرياض‎ ar-riyāḍ) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia.

Iko katikati ya Bara Arabu kwenye nyanda za juu za eneo la Najd. Kuna wakazi milioni 4.3 ambao ni karibu 20 % za watu wote katika Saudia.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mazingira ya Riyad ni jangwa lakini mahali penyewe pamekuwa na visima vya maji tangu karne nyingi kuna pia mvua kidogo. Siku hizi maji hupelekwa hasa kwa mabomba kutoka pwani penye vituo vya kuondoa chumvi kwenye maji ya baharini. Nyanda za juu hupokea kiasi cha mvua hasa wakati wa Aprili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Miji na vijiji vya mabonde yenye visima ya eneo la Riyad vilikuwa chanzo cha Saudia ya kisasa. Familia ya Saud ilitawala hapa tangu karne ya 18 na kujiunga na harakati ya Wahabiyya. Utawala huu ulivunjwa na Dola la Uturuki katika karne ya 19 lakini Wasaud walirudi mwaka 1902 na kutwaa boma la Riyad.

Abd al Azis Ibn Saud (1880-1953) alieneza himaya yake kutoka hapo baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (iliyoondoa Waturuki katika Uarabuni) kwa kushambulia na kutwaa maeneo mengine ya Bara Arabu na mwishowe Makka.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Riyad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.