Kiwelisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani yaonyesha asilimia ya wasemaji wa Kiwelisi kati ya wakazi wa Welisi

Kiwelisi (Kiwelisi: Cymraeg; Kiing. "Welsh") ni lugha ya Kikelti ya nchi ya Welisi kwenye kisiwa cha Britania jirani na Uingereza. Idadi ya wasemaji hukadiriwa kuwa kati ya watu 500,000 hadi 750,000.

Leo hi ni lugha ya Kikelti yenye wasemaji wengi. Katika Welisi ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza.

Kiwelisi kimejulikana kwa nafasi ya kuwa na majina marefu sana, kwa mfano Llanfairpwllgwyngyllgogerychwyrndrobwllllantysiliogogogoch (sauti ya jina hili lasikika hapa) ambacho ni jina la kituo cha reli kwenye kisiwa cha Anglesey.