Elimu ya watu wazima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Watu wazima wa Guinea-Bissau wakifundishwa nje ya jengo lolote, 1974.

Elimu ya watu wazima (au ya ngumbaru) huchukua maumbo mengi, yakiwemo elimu rasmi darasani, elimu ya binafsi na masomo ya mtandao.

Idadi fulani ya kozi za kazi maalumu, kama vile elimu ya mifugo, masuala ya madawa, uwekezaji, uhasibu na kozi nyinginezo kwa sasa hupatikana mtandaoni.

Elimu hii imekuwa kawaida katika nchi nyingi. Kwa muda mrefu Tanzania ilikuwa kielelezo kwa Afrika nzima.