Uhasibu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Uhasibu (kwa Kiingereza: accounting) ni upimaji wa hali ya kifedha ya shirika au biashara. Baada ya upimaji huo, mhasibu ana jukumu la kuwasilisha taarifa kwa wanaohusika.

Mfumo wa uhasibu unaofanyika hivi leo ulianzishwa na mwanahisabati wa Italia kwa jina Luca Pacioli mwaka 1494. Uhasibu, ambao wengi huuita 'lugha ya biashara', hupima matokeo ya kiuchumi ya shirika na baadaye kuwajulisha washika dau. Anayefanya kazi ya uhasibu huitwa mhasibu.

Uhasibu unaweza kugawanywa mara tano:

  • Uhasibu wa kifedha (financial accounting)
  • Uhasibu wa kimeneja (management accounting)
  • Ukaguzi kutoka nje (external auditing)
  • Uhasibu wa ushuru (tax accounting)

Uhasibu wa kifedha[hariri | hariri chanzo]

Uhasibu wa kifedha ni utengenezaji wa ripoti kuhusu fedha za shirika fulani. Ripoti hizi hutumika na watu wa nje ambao wangependa kuwekeza katika shirika lile au kulikopea .

Uhasibu wa Kimeneja[hariri | hariri chanzo]

Uhasibu huu hufanyika ili kuwezesha mameneja kufanya maamuzi kuhusu shirika.

Ukaguzi wa nje[hariri | hariri chanzo]

Ukaguzi wa nje au external auditing ni uhakiki kwamba yaliyofanywa na mhasibu ni kweli.

Uhasibu wa ushuru[hariri | hariri chanzo]

Uhasibu wa ushuru ni upimaji wa ushuru ambao shirika lafaa kulipa kwa serikali.

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uhasibu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.