Kidachi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kidachi ni neno la Kiswahili cha zamani linalosikika hadi leo katika sehemu za Tanzania kwa ajili ya lugha ya Kijerumani au tabia za Wajerumani. Neno limetokana na "Deutsch" (tamka: doitsh) ambalo ni jinsi Wajerumani wenyewe wanavyojiita.

Kidachi, Mdachi/Wadachi na Udachi yalikuwa maneno ya Kiswahili cha kawaida kutokana na utawala wa Kijerumani katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Tangu mwisho wa ukoloni wa Wajerumani mwaka 1918 na kuja kwa Waingereza wasemaji wa Kiswahili wamezoea zaidi kuwataja "Wadachi" kwa kutumia jina lenye asili ya Kiingereza, yaani Kijerumani, Mjerumani/Wajerumani na Ujerumani.

Mara nyingi maneno yenye "-dachi" huchanganywa na neno la Kiingereza "Dutch" linalomaanisha Waholanzi.

Kidachi kimeathiri kwa kiasi fulani lugha ya Kiswahili cha Tanzania bara kama vile kukikopesha maneno mbalimbali, kwa mfano: shule, hela n.k.