Visiwa vya Aland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Aland

Visiwa vya Aland (Kiswidi: Åland; Kifini: Ahvenanmaa) ni funguvisiwa ya Baltiki katika kusini ya Ufini yenye hali ya jimbo huru la nchi hiyo. Mji mkuu ni Mariehamn kwenye kisiwa cha Fasta Åland.

Ndani ya Ufini ni jimbo lenye utamaduni wa Kiswidi lililo na hali ya pekee kikatiba na kiwangi kikubwa cha kujitawala.

Funguvisiwa ina visiwa zaidi ya 6000 vingi ni vidogo sana na 60 pekee vina watu. Umbali na Ufini ni kilomita 15 na Uswidi ni 40 km. Kisiwa kikubwa ni Fasta Åland upande wa magharibi. Eeno la visiwa vyote ni 1,554 km². Jumla ya wakzi ni manmo 26,530.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1000 BK visiwa vilikuwa chini ya Uswidi. Wakati wa Uswidi kutawala Ufini vilihesabiwa pamoja na jimbo la Kifini la Uswidi. Tangu mwaka 1809 vilihamishwa chini ya Urusi pamoja na Ufini wote. Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kulitokea uhuru wa Ufini pamoja na fitina kama visiwa vitakuwa sehemu ya Ufini au ya Uswidi.

Shirikisho la Mataifa liliamua mwaka 1920 ya kuwa

  • visiwa vitabaki sehemu ya Ufini
  • wakazi wawe na uhuru wa kutumia lugha yao ya Kiswidi na kutunza utamaduni wao
  • visiwa viwe eneo bila wanajeshi

Ufini ilitekeleza azimio hili kwa sheria mbalimbali. Hivyo Aland ni sehemu ya Ufini ambako lugha rasmi ya pekee si kifini bali Kiswidi. Wafini kutoka bara hawaruhusiwi kununua ardhi au nyumba moja kwa moja kama hawakuishi visiwani kwa miaka kadhaa kwanza.

Finland stub POL.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Ufini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Aland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.