Lahore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Lahore
لاہور
Skyline ya Lahore لاہور
Skyline ya Lahore
لاہور
Majiranukta: 31°32′59″N 74°20′37″E / 31.54972°N 74.34361°E / 31.54972; 74.34361
Mkoa Punjab
Eneo
 - Jumla 1,772 km²
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 11,126,285
Tovuti:  www.lahore.gop.pk

Lahore (kwa Kiurdu: لاہور) ni mji mkubwa wa pili nchini Pakistan na mji mkuu wa mkoa wa Punjab. Inajulikana pia kama "Jiji la bustani" kwa sababu ya bustani zake nyingi. Mji huo unajulikana kwa utajiri wa utamaduni wake. Ni kitovu cha tasnia ya filamu ya Pakistan na hivyo kuitwa pia "Lollywood"

Maktaba ya Quaid-e-Azam katika Bustani za Lawrence, Mall, Lahore.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Lahore ina historia ndefu; ilianzishwa kama mji wa Uhindi ilhali tarehe haijulikani.

Baada ya uvamizi wa Waislamu katika karne ya 11 ilikuwa mara kadhaa mji mkuu wa milki za kieneo.

Wakati wa utawala wa Waingereza harakati ya kuunda Pakistan (kama nchi ya Waislamu kwenye Bara Hindi) ilianza hapa mwaka 1940. Wakati wa kugawanywa kwa Uhindi wa Kiingereza Lahore ilikuwa na wakazi Waislamu wengi, ingawa Wahindu na Wasikh walikuwa karibu nusu ya wote.

Baada ya azimio la kupeleka mji huo upande wa Pakistan kulikuwa na mapigano makali ambapo maelfu ya watu waliuawa, na wakazi wengi wasio Waislamu walikimbia upande wa Uhindi. Badala yao Lahore ilipokea wakimbizi Waislamu kutoka Uhindi.

Hata hivyo, leo hii bado wako Wahindu, Wasikh na Wakristo walio na mahekalu na makanisa yao ingawa si wengi, zaidi ya asilimia 90 ni Waislamu.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Lahore ni kitovu cha elimu ya juu cha Pakistan. Ina idadi kubwa ya taasisi za elimu kushinda miji mingine ya nchi. Chuo kikuu cha zamani cha Punjab kina kampasi mbili jijini. Taasisi nyingine za zamani na maarufu za masomo ya juu ni pamoja na Chuo Kikuu cha Serikali (GCU), Chuo cha Forman Christian na Chuo cha Kinnaird kwa Wanawake. Chuo cha kitaifa cha Sanaa, taasisi maalum ya sanaa nzuri kipo hapa pia.

Maisha ya kitamaduni[hariri | hariri chanzo]

Lahore ni moyo wa kitamaduni, wa fasihi na sanaa wa Pakistan. Inavyo vituo kadhaa maarufu vya kitamaduni kama Alhamra Theatre, Baraza la Sanaa la Punjab, Jumba la Lahore, Jumba la kumbukumbu la Shakir Ali, Jumba la kumbukumbu la Fakir Khana na Kikundi cha Theatre cha Rafi Peer.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lahore kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.