Punjab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya Punjab mwaka 1903
Punjab leo katika Uhindi na Pakistan

Punjab (pia: Panjab; Kipunjabi: ਪੰਜਾਬ panjāb, maji tano au nchi ya mito mitano) ilikuwa jimbo la Uhindi wa Kiingereza lililogawiwa tangu 1947 kati ya nchi za Uhindi na Pakistan.

Kijiografia ni tambarare ya mito mitano inayoingia katika mto Indus upande wa mashariki. Hali ya hewa ni yabisi lakini maji ya mito ni msingi wa kilimo cha umwagiliaji. Kilimo hiki chazalisha sehemu kubwa ya chakula cha Uhindi na Pakistan.

Panjab ni chanzo cha ustaarabu wa Uhindi wa Kale na maghofu ya Harappa yako hapa. Hadithi nyingi za maandiko matakatifu ya Uhindu kama Rig Veda, Upanishadi na Mahabarata yaliandiukwa hapa.

Asili ya dini ya Kalasinga iko Punjab.

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Punjab kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: